Ofisi ya Rais inapokuwa na Vitengo vya Mihimili

Hamatan

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2020
Posts
3,197
Reaction score
7,677
Mwalimu Nyerere alijua kuwa kuna haja ya kuwa na mihimii mitatu ya Jamhuri. Akalijenga Taifa katika mihimili mitatu yaani Serikali, Mahakama na Bunge. Japo muundo wake haukuashiria uhuru wa 100% lakini angalao iliachwa kuwa huru.

Utawala wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete, uliendelea kuheshimu uhuru wa mihimili hiyo, ndiyo maana Serikali mara kadhaa ilishindwa kesi mahakamani, Waziri Mkuu liweza kushinikizwa na Bunge, mpaka akajiuzulu.

Utawala wa Rais Magufuli, kwa vitendo vyake, ulifuta Bunge na Mahakama. Bunge na Mahakama vikafanywa kuwa idara za Rais, ambazo alizitumia kutekeleza anayoyataka yeye. Na akathubutu kutamka kuwa Urais ndiyo ulikuwa na mizizi, ina maana Mahakama na Bunge havina mizizi, akipenda anavinyausha kama apendavyo.

Akamteua jaji kukaimu nafasi ya Jaji mkuu kwa muda mrefu ili kumnyima confidence na uhuru wa maamuzi. Akamfanya Jaji mkuu na Spika kuwa miongoni mwa viongozi wa chama kwa kuwashirikisha kwenye vikao vya siri vya chama.

Mahakama ikabakia kuwa majengo ya kutekelezea maagizo ya Rais. Ndiyo maana aliposema anataka matajiri waishi kama mashetani, jeshi la polisi liliwakamata matajiri, DPP alitengeneza mashtaka bandia, mahakama iliwasweka ndani na kisha kuwakubalia watoe pesa ndiyo watoke. Polisi walipoua, wakaelekezwa kesi hiyo ya mauaji wapewe akina Mbowe, kisha walipishwe mamia ya mamilioni, na ikawa hivyo. Na majaji bandia wakateuliwa wengi kwaajili ya kutekeleza udhulumati. Hakuna aliyeishinda Serikali mahakamani, labda mtuhumiwa aombe msamaha, halafu mahakama inamwachia.

Ameingia Samia, hali aliyoiacha marehemu ni ile ile. Mahakama inaonekana inafanya kazi kwa maelekezo ya Rais. Aliposema hataki dhuluma, mahakama zile zile zilizowadhulumu, hizo hizo zikawaachia akina Mdude, akina Mbowe na matajiri ikaamliwe warudishiwe pesa zao, lengo likiwa kuitumia mahakama kuisafisha Serikali mbele ya uso wa mataifa lakini bila ya kuwa na dhamira ya kweli.

Hata kama Rais Samia aliweza kuitumia mahakama kutenda mema, hilo siyo la kufurahia. Kama alivyoitumia kutenda mema, ndivyo ana uwezo wa kuitumia kutenda uovu. Haionekana kama Rais Samia ana dhamira ya dhati ya kuitaka mahakama au Bunge kuwa huru, ndiyo maana hataki mchakato wowote wa kisheria utakaoifanya mihimili hii miwili, na ofisi ya DPP na CAG kuwa huru. Inaonekana Rais Samia anataka, kama alivyokuwa mtangulizi wake, na yeye aweze kuinyumbuanyumbua mahakama na bunge kama anavyotaka.

Katiba ni lazima, ili tuwe na Mahakama, Bunge, ofisi ya CAG na DPP, zilizo huru, na siyo hizo zinazolazimishwa zidemka kama anavyotaka Rais.
 
Hapo unaona kwamba kutokana na Katiba mbovu tuliyonayo, watanzania tunaishi kwa kutegemea kudra za mtawala, akiamua kutulambisha mchanga wote tutaulamba bila kujali itikadi za vyama vyetu, na akiamua kutulambisha asali pia wote tutailamba.

Niwashauri tu wale waimba mapambio wa Lumumba, nao waamke tuungane kuidai Katiba Mpya itakayotufanya wote tuifurahie Tanzania yetu bila kujali vyama vyetu, leo tunaumizwa na tozo za miamala ya simu, hizi tozo hazichagui CHADEMA, CCM wala CUF.
 
Wanaouliza kwa nini Mbowe amekamatwa sasa na si vinginevyo wanasahau kuwa Mbowe, Lema, Meya wa zamani Ubungo Boniface walikamatwa mara baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu kutangazwa na kabla Rais hajaapishwa kwa kuchochea maandamano yasiyo na kikomo kupinga matokeo. Mambosasa alihojiwa na vituo vya ITV na TBC na kutoa madai hayo hayo ya ugaidi.
 
Katiba kuipata itatuchukua muda mrefu kwasababu mpaka Rais aridhie.Na hakuna cha kumfanya kwani ana kinga yakutokushitakiwa.

Ushauri;
Iwe hoja ya dharula kuifuta sheria ya KINGA kwa viongozi. Hakika hata hii katiba iliyopo mtaiona bado inafaa.
 
Hapo unaona kwamba kutokana na Katiba mbovu tuliyonayo, watanzania tunaishi kwa kutegemea kudra za mtawala, akiamua kutulambisha mchanga wote tutaulamba bila kujali itikadi za vyama vyetu, na akiamua kutulambisha asali pia wote tutailamba.

Niwashauri tu wale waimba mapambio wa Lumumba, nao waamke tuungane kuidai Katiba Mpya itakayotufanya wote tuifurahie Tanzania yetu bila kujali vyama vyetu, leo tunaumizwa na tozo za miamala ya simu, hizi tozo hazichagui CHADEMA, CCM wala CUF.
Wana-CCM kama wanadhani wapo salama, wajifunze kutoka DRC, Uganda na hata Zambia. Wajifunze namna Chiluba, Mobutu na Amin walivyotumia katiba zao mbaya kuwadhibiti watawala wa mwanzo.

Hapo Zambia, wapinzani chini ya Chiluba, waliomba sana mabadiliko ya katiba ili kupunguza mamlaka ya Rais. Mzee Kaunda na chama chake cha UNIP walikataa katakata.

Mara Chiluba akawa Rais. Naye hakubadilisha katiba. Akaitumia katiba ambayo Kaunda alikataa kuibadilisha, akamweka ndani Kaunda. Kaunda alitolewa baada ya miezi kufuatia ombi la Mwalimu Nyerere.

CCM kuna siku watatoka madarakani, wataingia wengine, nao wataitumia katiba hii hii mbaya kuwaadabisha CCM. Watajuta. Kama ndani ya CCM kungekuwa na wenye akili, kwa makosa mengi waliyoyafanya, wao ndio wangekuwa vinara wa kutaka katiba mpya, ili kikija chama kingine, Rais asitumie madaraka yake vibaya dhidi yao.
 
Asante sana.
 
kwa sababu wana mtazamo finyu hawawezi kuelewa, wanajiaminisha kwamba wao ndo watashinda hadi milele......na kwa sababu rais anatokea kwenye chama chao wataendelea kula bata, nafikiri kuna funzo walipata kwa mwendaa......kwamba binadamu hatabirii......
 
Back
Top Bottom