KERO Ofisi ya Rais Utumishi ni kero kuhusu hamisho kwenye mfumo wa ESS

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Serikali ya Jamhuri ya Muungano kupitia ofisi ya Rais- Utumishi ilianzisha mfumo wa ESS ambao umerahisisha shughuli nyingi za kiutumishi, moja ya suala lililorahisishwa ni ushughulikiwaji wa uhamisho wa Watumishi kwa njia ya mtandao. Cha ajabu ni kwamba Watumishi walioidhinishiwa hamisho zao na waajiri wao , hamisho zao zimekwama ofisi ya Rais- Utumishi.

Mfano binafsi uhamisho wangu uko Utumishi kwa miezi mitano sasa na nimefanya juhudi zote lakini sijafanikiwa. Uzuri mfumo mpya wa ESS unaonesha ni wapi uhamisho ulikokwama.

Inashangaza kila siku Waziri wa Utumishi mhe simbachawene anazingumzia kuhusu kutokuwakwamisha watumishi kuhama wakati ofisi yake ndiyo inayokwamisha. Utumishi imegeuka kero.

Pia kuna watumishi wanaofuata wenza wao, ulitoka waraka ili wahusika wajaze taarifa zao waweze kuhamishwa, suala hili pia limekwama tangu septemba 2024 na limekwamia Utumishi.

Mhe simbachawene anapowaelekeza wakuu wa taasisi kuhusu hamisho huwa haelewi kwamba tatizo ni ofisi yake ??
 
Ulishajaribu kuwafuata kuwauliza kwann haujibiwi maombi yako??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…