Ofisi ya Rais yatofautiana na Waziri Bashe suala sukari

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
OFISI ya Rais, Mipango na Uwekezaji imetofautiana mtizamo na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwenye kampeni yake ya kuhamasisha utoaji wa vibali vya kluagiza sukari kutoka nje.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo ametoa kauli hiyo mjini Dodoma na kusisitiza kuwa mipango iliyopo ya uboreshaji wa viwanda vya sukari inakwenda vizuri na kwamba kufikia mwakani 2025 nchi yetu itajitosheleza kwa sukari na hatutaagiza tena sukari kutoka nje.

Kauli ya Ofiisi ya Rais imekuja siku chache baada ya Bunge kupitisha Sheria ya Fedha iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Kilimo na Waziri wa Fedha kuruhusu watu binafsi kuagiza sukari nje ya nchi na kutishia uhai wa viwanda vya sukai nchini.

PIA SOMA
- Umoja wa wazalishaji wa sukari Tanzania (TSPA) Wajitetea kuhusu kupanda kwa Sukari. Hawajawahi kuficha Sukari, Si kazi yao kuagiza Sukari nje

Your browser is not able to display this video.
 
Ukweli utabaki ukweli kwamba Viongozi wooote, wa Awamu iliyoko madarakani, ni kambale: hawaheshimiana, wanatumia madaraka kujineemisha, hawaheshimu mamlaka yaliyo juu yao, na hawajali na hudharau wanaowaongoza
 
OFISI ya Rais, Mipango na Uwekezaji imetofautiana mtizamo na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwenye kampeni yake ya kuhamasisha utoaji wa vibali vya kluagiza sukari kutoka nje...
uwezi sikia watabishana hiyo inaitwa no VAR
 
OFISI ya Rais, Mipango na Uwekezaji imetofautiana mtizamo na Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwenye kampeni yake ya kuhamasisha utoaji wa vibali vya kluagiza sukari kutoka nje...
Ngoma bado mbichi
Sukari itaondoka na mtu
Awe bashe awe mwigulu au mama sbdul
 
Bashe anataka watu binafsi waagize sukari nje na Ofisi ya Rais inataka viwanda vijitosheleze kuanzia mwaka kesho.
Bashe ameisha nogewa na rushwa ya vibali,

Wasawahili husema mpe mtu madaraka na fedha tujue tabia yake

Bashe tuliyedhani ni mwenzetu kashatigeuka tayari
 
Bashe anaongea uhalisia, Mkumbo anaongea siasa as usual. Hao watu wangetaka tujitosheleze sukari uwezo huo wanao. Hawafanyi hivyo ili wapige super profit kwenye kuagiza.
 
nadhani wewe ndie unaeconfuse mambo ya mpango wa dharura na mpango endelevu wa kujikwamua na dharura na kujitegemea uzalishaji na utoshelevu sukari nchini 🐒
 
Ukweli ni kwamba! CCM kula rushwa ni sawa na mtu kumeza almas

Msema kweli CCM ni sawa na mtu muovu, kwao ccm mtu huyo anapaswa anyongwe hadi afe kama wanavyomfanya Mh. Mpina
 
Bashe anataka watu binafsi waagize sukari nje na Ofisi ya Rais inataka viwanda vijitosheleze kuanzia mwaka kesho.
Sisi Wananchi tunachotaka ni Sukari na ya bei nafuu.
 
Bashe muda huu alitakiwa awe mahabusu kama ni china keshanyongwa kitambo hata familia imeshamaliza matanga!
 
Bashe anataka watu binafsi waagize sukari nje na Ofisi ya Rais inataka viwanda vijitosheleze kuanzia mwaka kesho.
Sioni kutofautiana kwa kauli.
Bashe kazungumzia tahadhari kwa yaliyotokea 2024 (kwa mfano mvua za El-nino). Hayo yanaweza kutokea wakati wowote hata kama mlishajipanga kuwa ktk karatasi uzalishaji unatosheleza.
Waziri mkumbo kajikita kwenye mpango wa serikali na viwanda katika uwezo wa uzalishaji kama hakutatokea ajali yeyote.
Hapo tofauti ipo wapi? Ndugu zanguni acheni ushabiki katika suala la SUKARI.
 
Ukitumia akili za kuambiwa ukachanganya na zako, unaona ukweli wa jambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…