NYENJENKURU
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 1,066
- 294
Ndugu wanaJamvi kuna jambo limenishangaza kidogo kutoka ofisi ya RITA MISSENYI mkoani Kagera.Kuna mtoto wa shemeji yangu aliomba cheti cha kuzaliwa kwa njia ya mfumo wa RITA ajaza kila kinachotakiwa kuwekwa kwenye mfumo.Baada ya wiki moja kwenye mfumo status ikaonyesha Cerificate Issued,Collect your cerificate at RITA office Messenyi.MAAJABU walipoenda kuchukua cheti wakaambiwa kweli kimetoka na wakawaonyesha ila wakaambiwa kwa utaratibu wao RITA Missenyi ni lazima kwanza uje wakuone na baada ya hapo unapewa siku mbili ndo uje ukichukue . Wameenda leo(23/5/2024) kuchukua wameambiwa warudi Jumatatu(27/5/2024) kweli hii ni HAKI au wanatengeneza mazingira ya kulamba Asali?