Ofisi ya Shule ya Msingi Chini ya Mti Huu…!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Mti huu kivuli chake ni ofisi ya walimu (staff room) wa Shule ya Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe. Thehabari.com imelazimika kuitembelea tena shule hii ikiwa ni miezi sita baada ya kuitembelea awali mapema mwezi Agosti 2012.

Hili ni darasa jipya lililojengwa sasa katika Shule ya Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe, darasa hili linatumiwa na wanafunzi wa darasa la tatu. Lakini nje kivuli chake wakati wa jua kali ni ofisi ya walimu wa shule hiyo.

Madawati haya mbele ya darasa hili ni Ofisi ya walimu (staff room) katika Shule ya Msingi Silabu, husogezwa hapa baada ya kivuli cha mti kutoweka katika mti ambao hutumika kama ofisi shileni hapo.

Uchochoro huu awali ndio ulitumika kama darasa la tatu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Silabu iliyopo Wilaya ya Korogwe. Jitihada za Serikali zimefanywa na sasa limejengwa darasa moja ambalo linatumiwa na wanafunzi wa darasa la tatu. Thehabari.com imelazimika kuitembelea shule hii tena ikiwa ni baada ya kipindi cha miezi sita. Awali (Agosti 2012) iliripoti wanafunzi wa darasa la tatu kusomea uchochoroni baada ya kutokuwa na darasa.

Choo hiki cha Shule ya Msingi Silabu kiliezuliwa na upepo muda mrefu sasa lakini kutokana na hali ngumu ya bajeti ya fedha bado hakijarekebishwa, Serikali inafanya juu chini kufanikisha hili itakapopata fungu la kutosha.

Short URL: Ofisi ya Shule ya Msingi Chini ya Mti Huu…! | Blogs Tanzania | News | Michuzi ya Habari leo
 
-serikali haina fedha kwa sasa-TRA imevuka lengo la ukusanyaji kodi-malori 26 yamelipiwa ushuru 16m tuu-rais yupo US
 
Hakuna shule nzuri kama hii, maana msimu wa mvua tunafunga shule. Mungu wangu Korogwe hapo nyumbani kabisa, eti wana Mbunge mmmhhh eti ndio madarasa haya Kaka Alfani alisema yawe yanatumia Laptop na Teleconference kufundiishia ili kupunguza tatizo la uahaba wa walimu.

Hivi vile vipindi vya shule kwa njia ya Radio vilivyoanzishwa na Kapuya bado vinaendelea kweli? Mbona siiioni redio ya walimu ya kufundishia??? Vitu vingine ukifuatilia sana waweza pata kiskuari
 
Kutokana na hali hii niliyoiona kwa picha hii, napenda kumwandikia Naibu Waziri wa Elimu Mh Philipo Mulugo afanye kila linalowezekana kuwapa BONUS Walimu wa Shule hii kwa MOYO MKUU WA KUFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU. Hongera sana walimu wote wa Shule hii kwa MOYO WENU WA UALIMU. Hakika UALIMU NI WITO
 





Chama chetu tawala kinajitahidi kutimiza ahadi zake na ilani ya uchaguzi kwa wananchi wake,that is the best of our Government.Duh Tanzania zaidi ya uijuavyo,natamani hii picha aione Nape!!!!!!!!!!
 
Jamani yeyote anayeweza kuwasiliana na Mh Philipo Mulugo wamweleze kisa hiki. Najua zipo shule nyingi sana zilizo katika mazingira kama haya. Malaria zinatofautiana makali kulingana na maeneo na tabia nchi. Miaka 50 ya Tanzania huwezi amini kama kuna Shule za nyakati za UJIMA kama tunavyoiona shule hii. Ili kuonyesha UZALENDO kwa Moyo wa WITO wa Walimu wa Shule hii Serikali ifanye kila linalowezekana kuwazawadia ASANTE YAKE KWA VITENDO. Tusiwafanye walimu hawa kama ni watu walioumbwa kuwa na matatizo. Walimu hawa wameishi kwa VITUMBUA NA VISHETI. Mh Philipo Mulugo natambua sana umekuwa ukihangaika huku na huko kufuatilia mambo ya elimu hapa nchini. Tupia jicho lako huko Mh. Mulugo wewe usubiri kura kwa wananchi wako jimboni. Wanayofanya akina Mwakyembe na Magufuli ni haya mambo yanayoigusa sana jamii kwa upande wako Mh. Philipo Mulugo hapa tenda WEMA KWA WALIMU HAWA. Jema utakalo fanya kwa walimu hawa Mungu hatakunyima kura 2015.

Unapooa ukaona Mke ameweza kuvumilia maisha magumu ya ndoa yenu tangu siku ya awali kwa kulala chini, kula mlo mmoja, kuvaa kanga yenye viraka, kutopata maboresho ya saloon na kadhalika, kama wewe mume una moyo wa dhati kwa mkeo,,,,,, huwezi kamwe kumuacha siku ile mambo ya kimaisha yatakapokuwa bora zaidi. Maisha magumu waliyoishi walimu wa shule hii bila shaka yametikisa hata maisha yao ya ndoa na hili ndilo linalonifanya nione KUWA WALIMU HAWA WANA WITO WA KAZI YAO. Kazi kwako Mh. Mulugo.
 
Mh Mulugo yeye anafuatilia shule za binafsi tu zingine hazimhusu.
HAWA WANA MBUNGE NA ANAPEWA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO?
 
Nikikumbuka wapo wanaosoma St. Marys', St. Methew, Christ Tha King, St. Marian Girls, Mzumbe, Umbwe, Illboru, Malangali, Songea Boys/Girls, Weruweru, Seminaries zote nchini, Tambaza, Jangwani, NK

KISHA NIKILINGANISHA NA SHULE KAMA HIZI AMBAZO WANAFUNZI WAKE NI WATOTO WA WATU WALIOPORWA UTAJIRI WAO, SIPENDI KUITA WATU MASIKINI, KAMWE MSEMO HUU UNATUTIA HASIRA SANA SISI WATANZANIA CHANZO CHA UMASIKINI SI KINGINE NI SERA MBOVU KABISA ZA SERIKALI KUHUSU MALI ASILI ZAO IKIANZIA ARDHI NA KADHALIKA.

TUNAOMBA SANA MAWAZIRI, WABUNGE ACHENI KUTUITA SISI NI WATOTO MASIKINI. WEWE UTAJIRI UMEUPATA WAPI KAMA SI KWANJIA YA KUTUNYONYA SISI????????

STOP CALLING US POOR FAMILY CHILDREN AND YET YOU LEAVE US LIVING SUCH A POOR LIFE STARTING POOR SCHOOLS DIRTY WATER POOR HOSPITALS ETC.

STOP YOUR "UMASIKINI WETU UMETUFIKISHA HAPA" PROPAGANDA
"ARE YOU LEADING US TO POVERTY???"
 
View attachment Poor school.bmp

Mazingira magumu haya ninyi viongozi mpo mnaishi kwa raha mstarehe, je ninyi ni watu mlioumbwa kama sisi mnaotuita masikini? Mh. Kinana juzijuzi ulipiga marufuku hili neno "MHESHIMIWA" Kwa makusudi mnatumia neno UMASIKINI katika majukwaa yenu bila kujua ATHARI ZAKE KWENU na kwetu. Neno hili ni sawa na Mzazi kumuita mwanae "Chausiku, Tabu, Logeni, Matatizo, Majuto, Wasiwasi, Mawazo, Nia gani, Sikudhani, Fitina na kadhalika" athari ya majina haya kwa mhusika mwenye jina ni kama yanavyosomeka, Chausiku atakuwa hatulii kurudi kwake ni asubuhi yeye na wanaume tu, Tabu yeye maisha yake yataakisi tabu iliyoko mbele yake, Logeni yeye kila analofanya asipopata mafanikio atatangaza kalogwa, Matatizo kama alivyo tabu yeye huyu atakuwa ni mtu mkorofi akipigana ovyo ovyo na wenzake, Majuto atakuwa ni mnyonge kila mara kwa kutofanikiwa kwake, Wasiwasi ni mtu atakaye ishi kwa hofu ya kutojua kesho atakula nini na mara nyingi hawa ndiyo wale tunaowakuta mitaani wakiwakaba watu kutatua shida zao. Sipendi kuendelea kuandika mengi kwani nitawafanya wasomaji wasipende kusoma mada ndefu.

Mnapotuita "WATU WA FAMILIA MASIKINI, JUENI YA KUWA NINYI NDIYO CHANZO HASA CHA KUTUFANYA TUWE HIVYO,
KUNA MSEMO UNAOSEMA ADUI YAKO MUOMBEE NJAA, SERIKALI ILI IENDELEE KUTUTAWALA NA SI KUTUONGOZA YENYEWE INASEMA "MWANANCHI ILI UWEZE KUMTAWALA MPE ELIMU MBOVU.

KUNA WAZIRI ANAITWA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS NA UTAWALA BORA, FUTENI NENO UTAWALA WEKA WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS NA UONGOZI BORA. MMEENDA HUKO KUTUTAWALA AMA KUTUONGOZA???

WAKOLONI WALIKUJA KUTUTAWALA NINYI BAADA YA UHURU HAMTUTAWALI BALI MNATUONGOZA TAFADHALI BADILIKENI KIFIKRA.

DO YOU WANT TO ASSURE US THAT YOU ARE AGENTS OF COLONIALISM???

please your party is ruling but you are leading us PLEASE YOUR PARTY IS RULING BUT YOU ARE NOT A RULER YET YOU ARE A LEADER, LEADING US.

WHAT DOES A RULER DO? AND WHAT DOES A LEADER DO?

KWA NINI MNATUCHANGANYA HIVI.

TULIAMBIWA KUWA ILI TUENDELEE TUNAHITAJI VITU VINNE
1. WATU
2. ARDHI
3. SIASA SAFI
4. UONGOZI BORA (SIYO UTAWALA BORA)
 
Inauma sana! Halafu walimu hawa wakilalamika wanajibiwa vibaya,majengo duni kazini mpaka wanakoishi! Mishahara duni,kwa hali hii ile chain ya umasikini inazunguka tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…