Ofisi ya uhasibu saut inavyogharimu wanafunzi dhidi ya mikopo yao.

Ofisi ya uhasibu saut inavyogharimu wanafunzi dhidi ya mikopo yao.

don-oba

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Posts
1,387
Reaction score
677
Kwa mara nyingine tena ofisi ya uhasibu imefanya madudu mengine na kuwagharimu wanafunzi zaidi ya 500 ambao hadi sasa hawajapata mikopo yao. Tangu kuanza kwa mwaka wa masomo baadhi ya wanafunzi hawajapata pesa zao kwa uzembe mkubwa uliofanywa na ofisi hii kushindwa kupeleka matokeo ya wanafunzi. Kwa jeuri na kiburi mhasibu anayejulikana kwa jina la MUSSA alikua akiwajibu wanafunzi kwamba tayari ameishatuma majina bodi ya mkopo. Wakati ilitakiwa awe ametuma majina hayo tangu mwezi sept mwaka jana imekuja julikana kwamba ametuma hayo majina juzi tar 8/1/2013!. Leo hii saa 2 usk kupitia STAR TV mtaona malalamiko ya wanafunzi juu ya uzembe wa uongozi wa juu kushindwa kumtimua Mussa pamoja na kuwa anawaletea migogoro ya kila mara.
 
Back
Top Bottom