Ofisi ya Waziri Mkuu imekagua mradi wa bidhaa za ngozi eneo la Karanga, Moshi

Ofisi ya Waziri Mkuu imekagua mradi wa bidhaa za ngozi eneo la Karanga, Moshi

Nancyjoa13

Senior Member
Joined
May 18, 2018
Posts
167
Reaction score
97
1589705258789.png


Ofisi ya Waziri mkuu imeziagiza Jeshi la Magereza nchini na Mfuko wa hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),zinazotekeleza kwa pamoja mradi wa zaidi ya shilingi bilioni 75 wa kiwanda cha bidhaa za ngozi eneo la Karanga,Moshi,Mkoani Kilimanjaro,ambao umefikia asilimia 95 kuhakikisha wanakamilisha kwa wakati miundombinu ambayo badokukamilika ili kiwanda kianze uzalishaji mara moja.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. ANDREW
MASSAWE,ametembelea mradi huo na kutoa maagizo matatu kwa pande mbili zinazotekeleza mradi huo ikiwemo kuhakikisha vifaa vya umeme vilivyoagizwa kwa kampuni za ndani vinapatikana na mkazo mwingine kuhusiana na ulinzi hususani wa mashine ambazo tayari zimeshawasili kufutia gharama yake kubwa.

Katika Hatua nyingine wakuu wa Taasisi wabia katika mradi huo,wametoa mitazamoa yao kufuatia maagizo ya Ofisi ya waziri mkuu.

Matarajio ya kiwanda hicho cha kimkakati ambacho ni upanuzi wa kiwanda cha sasa kinachozalisha jozi 400 za viatu kwa siku,zikiwemo buti za jeshi na kiraia,ni ,kuzalisha jozi 4,000 za viatu vya kiraia pekee kwa siku sawa na takribani jozi milioni 1.2 kwa mwaka kikiratajiwa kuzalisha jumla ya ajira 7,000.
 
Jeshi la Magereza Wameanz kuonekana wanafanya kazi sasa maana hicho kiwanda kilikuwepo ila utendaji kazi wake haukueleweka wazi
 
Back
Top Bottom