Ufunguzi wa mafunzo ya Vijana juu ya stadi za kushona na kukata vitambaa kutumia teknolojia ya kisasa katika kiwanda cha Mazava Fabric Co.Ltd Morogoro leo ambapo takribani vijana 1000 watapatiwa mafunzo na kuajiriwa baadaye.
Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira inatarajia kukuza ujuzi kwa vijana takribani 27,000 kwa mwaka wa fedha 2016/2017 katika sekta mbalimbali za uchumi ili kuiandaa nguvu kazi ya nchi kushiriki kikamilifu katika uchumi wa viwanda.