Ofisi ya waziri mkuu na makamu wa raisi zataka serikali tatu

Ofisi ya waziri mkuu na makamu wa raisi zataka serikali tatu

SUBE2021

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2011
Posts
348
Reaction score
101
Nilipendezwa sana niliposikia kuwa hata ofisi ya Mh. Waziri Mkuu na Makamu wa Rais zilipendekeza Serikali Tatu. Hawa ni watumishi wa umma wanaostahili kupongezwa kwa kuuona ukweli wakiwa sawa na Ofisi ya Balaza la wawakilishi ambayo nayo niliwahi kusikia walipendekeza hivyo.

Hivi tujiulize leo tunapopata rais anayetoka Zanzibar kuwa wa Muungano na yule wa Zanzibar akawa Mzanzibari hatuoni hata hapo kuwa kunakuwa hakujakaa sawa.

Big up watanzania wote tunaounga mkono serikali tatu, si kwamba hatutaki muungano bali tunataka muungano ulioboreshwa. Na ili Muungano uwe bora kuna njia mbili Serikali moja au tatu sasa ni kupima kati ya miundo hiyo ni upi wengi wanautaka.
 
Wapo walotaka Warioba apewe dakika chache ili tusisikilize yote aliyokuwa nayo. Nawashangaa nilioona kwenye kipima joto wanalaumu wabunge waliosimama kupiga kelele kutaka Warioba siku ya kwanza asiendelee kusoma. Wanaolaumu hawakujua msingi wa wabunge kufanya hivyo sasa tumeona wenyewe jinsi Warioba alivyopata muda wa kutosha kuwasilisha
 
Namsifu Warioba kwa kukiwasilisha kile ambacho wananchi wengi wanakitaka. Kama Muungano uendelee kuwepo hatuna budi kuwa na serikali 3, Z'bar wenzetu wanayo tayari na rais wao, je serikali ya Tanganyika iko wapi na rais wake? Mh. Rais J. Kikwete ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kama itashindikana serikali 3, basi serikali moja na ile ya Z'bar ikivunjwa. Je wazanzibari watakubali?
Hapo ndipo tunarudi kwenye maneno ya Mh. Warioba kuwa ''Serikali 3 haziepukiki''.
 
Kinachowachanganya CCM ni neno raisi. Nchi nyingi za muungano duniani kila component inakuwa na serikali yake then kunakuwa na federal government...
 
Back
Top Bottom