TRA Tanzania
Senior Member
- Jul 16, 2022
- 128
- 370
Dar es Salaam, 07 Juni, 2024:
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), inapenda kuwafahamisha Walipakodi na wananchi kwa ujumla kuwa, ofisi za TRA nchi nzima zitakuwa wazi kuwahudumia walipakodi siku ya Jumamosi tarehe 08 Juni, 2024 na Jumapili tarehe 09 Juni, 2024 kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa 8:00 mchana.
Hatua hii inatokana na ushauri na maoni ya wadau wa kodi wakiwemo walipakodi wetu, hivyo TRA inawakaribisha walipakodi wote kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali za kikodi katika muda tajwa hapo juu.