Utangulzi:
Kumekuwa na ukimya mwingi juu ya lini ofisi kuu za ubalozi zitahamia Dodoma ili ofisi za Dar es Salaam zibakie kuwa ofisi ndogo. Hivyo nimekajaribu kuwaza nikafikiri kuwa kuna haja ya kulitizama hili ili kuamsha hisia kwa wahusika na kujua mipango ama viashiria vya changamoto katika kufikia malengo hayo ya kuhamia Dodoma.
Kuna Mipango gani ya Serikali
Ni lini ofisi za Balozi za nje zitahamiia Jijiini Dodoma. Uzuri serikali na karibu taasisi zote kubwa zimehamia Dodoma. Ofisi na makazi ya mabalozi zitakuwa zimekamilika kujengwa hadi kufikia 2025?
Kuna haja ya kukaa na mabalozi ama wakuu za mashirika ya kimataifa yenye hadhi ya UN na kuskia mahitaji yao na kujua changamoto zao katika kufikia kukamilisha ujenzi wa ofisi zao hadi kufikia 2025?
Kuna haja ya kuwakutanisha mabalozi na kampuni za ujenzi ili kushirikishana nao juu ya namna nzuri ya kufanikisha ujenzi pengine na kufanya maonesho ya ramani ama makisio ya gharama ama uwezo wa kampuni za ndani kama bidhaa wanazoweza kuziuza?
Kama ofisi za Balozi zingine zitaongezeka, maeneo bado yapo ya kutosha kwa ajili ya kugawa na kuongeza ofisi za balozi mpya?
Kuna haja ya kutoa muda maalum kwa balozi zilizopewa maeneo ya kujenga ofisi zao kuanza kuyaendeleza maeneo husika ama lah yarudishwe serikalini kwa kushindwa kuyaendeleza?
Viashiria vya ofisi za mabalozi kuchelewa kuhamia Dodoma
Miundombinu kama hospitali, shule, hoteli ili kutosheleza mahitaji ya hadhi zao, watumishi wao ama wageni wao. Upatikanaji wa maji safi yakutosha? Umeme wa kutosha? Usalama wa kutosha wa watu na mali zao?
Usafiri wa uma na binafsi na unaofikika katika maeneo tofauti kirahisi kama Reli, Uwaja wa ndege, Daladala na Taxi (Uber, Taxify, Bolt) nk ili kuchochea urahisi wa mawasiliano na kulifungua jiji la Dodoma?
Changamoto ya upatikanaji wa raslimali fedha kutoka serikali za Balozi husika. Pengine mchakato kwa nchi husika unatakiwa kuanzia bungeni ili bajeti itengengwe na fedha ya ujenzi ipatikane?
Upatikanaji wa nyumba za kupanga za makazi kwa maafisa ubalozi na watumishi wengine wa ofisi hizo za ubalozi katika jiji jipya la Dodoma
Mapendekezo
Haja ya kuunda timu ya wizara ili kufuatilia changamoto za ofisi moja moja za ubalozi na kutoa taarifa kwa Waziri/Katibu Mkuu kila mwezi ili pamoja na mambo mengine ajue nini kinaendelea na wapi kuna changamoto kubwa katika kufikia malengo ya kuhamia Dodoma
Upatikanaji wa viwanja vya gofu, majumba ya sinema, migahawa, maeneo salama ya kufanya mazoezi kwa mfano kukimbia, kutembea, bustani za wazi: je, yameshaanza kuandaliwa katika eneo ama Jirani na ofisi za balozi?
Kuipitia tena ramani ili kuona huduma ama shughuli zinazopatikana jirani ama kuzunguka maeneo ya ofisi za balozi: kuona kama yanachochea usalama wa ofisi na makazi ya watu

Upvote
2