Ofisini kwetu wananifanya mimi kituko

Ofisini kwetu wananifanya mimi kituko

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Kuna muda nakaa chini natafakari na kujiuliza why me yaani kila napokuwepo lazima kutatokea kitu ambacho kitanifanya nikose raha.

Kuna ofisi nipo nimejishikiza hapa mjini ila staff wenzangu wamenifanya mimi kama kituko wananidhihaki kwa kigezo cha utani yaani kila niwapo ofisini uanzisha mada za kuniponda na kuniona mimi wakuja na toka nilivyowaambia nimetokea Namtumbo wameacha kuniita jina langu wananiita Namtumbo.

Juzi nilisahau chaja nyumbani nikawaomba chaji nichajie kwa makusudi kabisa wakanipa charger type c sasa mi nilikuwa sijui kama ni type c nikawa naforce kuchajia wakaanza kunicheka siku nzima topic ilikuwa ni mimi sijui type c.

Jana kuna mtu alivua viatu ofisini kiukweli miguu yake ilikuwa inatoa harufu wote wakanikomalia kuwa ni mimi ndio viatu vyangu vinanuka.

Leo wamekuja na topic kuwa mimi ni mkubwa sana inaonekana ujanani mwangu nilichezea pesa kwenye ulevi maana sura yangu imekaa kilevi levi so wamenitolea mfano kama mtu niliyekosa ramani ya maisha ilibidi nikae kimya mwishoni wanaanza kusema Namtumbo usikasirike huu ni utani tu.

Sasa kuna siku nitatoka home nimevuta nahisi ndio mwanzo wa mwisho wa staff wenzangu kunizoea kiboyaboya.
 
a3390e92-704f-45cc-924b-fa173db4b29d.jpg
 
Back
Top Bottom