Ogopa kama ukoma wanawake wanaokuambia fulani (Rafiki yako) kanitongoza

Ogopa kama ukoma wanawake wanaokuambia fulani (Rafiki yako) kanitongoza

100 others

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2017
Posts
4,766
Reaction score
16,191
Wakuu habari za majukumu?

Wanaume wenzangu huwa inatokea sana kwenye mahusiano kuambiwa na mwanamke uliyenae katika mahusiano "kaka yako kanitongoza" au "rafiki yako ananitongoza", kwa kweli nimejifunza mengi kutoka kwa hili na ninaongea nina uhakika.

Wanawake wana tabia ya ku manipulate akili zetu, that is the only way kwa wao kutu control, wanawake wanachezea sana akili zetu and natuarally wapo hivyo so kama we upo katika beginner level utakubali show.

Mwanamke wa type hii anakuambia hivyo ili.

1-Utengeneze trust kwake kwamba yeye ni mwanamke wa shoka anajua kukwepa mishale, pia haoni mwanaume kama wewe.

2-Anatengeneza uadui kati yako na huyo mtu kwa sababu fulani fulani ili atimize mambo yake.

Huyo mtongozaji anaweza kuwa rafiki yako, ndugu yako au jirani yako, sikatai kweli kuna viwembe wa kula mali za watu lakini kuna namna ya ku solve issue kama hii.

Uzoefu ninao na kwa mifano halisi.

Naongea hili nina uzoefu nalo, mwanamke mwenye msimamo na anayekupenda kweli, asiyetaka ugombane na watu akitongozwa na wanaume wengine ambao kwa namna moja ama nyingine una mahusiano nao kama ndugu au marafiki inabidi yeye mwenyewe asimamie hilo, kwa kuwajibu "nitamwambia boyfriend wangu ukiendelea kunitongoza, naomba unikome mimi sio malaya, ukithubutu tena nitamwonyesha sms zote na nitamwambia".

Hapo midume lazima iogope ni kama pepo limekemewa, lakini wanawake wengi wana hizi tabia anatongozwa na watu wa karibu, halafu ana respond vyema, jamaa anapata nguvu zaidi ya kurusha mashambulizi, sisi wanaume ukiwa unatongoza halafu unaona mdada anaangalia chini huku kakaa kimya hapo unapata nguvu na kuendelea kutoa dozi kwa maneno, ndio maana unakuta mtu anasema " nitakununulia V8 mama" tena kwa ujasiri wakati hata pikipiki uwezo hana. Kwa sababu wanaume tunaamini ukimya nalo huwa ni jibu.

Sasa mwanamke akishadanganywa vya kutosha na akamkubalia jamaa cha kufanya ni kukugombanisha nae rafiki zako ili akiliwa usijue.

1-Hutoamini kama mwanamke wako itatokea siku akatoka na jamaa kwa sababu mwanamke amekuaminisha ana msimamo kwa kukuambia ametongozwa na huyo mtu.

2-Hutopata taarifa zozote kwa sababu mwanamke amaekata mawasiliano kati yako na huyo mtu na wengine.
Hapo hasara mara mbili.

1-Manzi analiwa.
2-Mahusiano na undugu/urafiki unakufa.

Pia kuna wanawake huwa wanakuja katika maisha yako wanakuta mna umoja, mna michongo yenu, una rafiki wengi na una mapenzi na ndugu zako, wakija na tamaa zao ili kutimiza adhma yao ndio huwa mbinu zao.

1-Kuhakikisha urafiki na undugu wenu unakufa ili akiwa ana cheat asipatikane wa kukupa feedback kwa sababu mmegombana nao.
2-Kukufanya umwamini yeye kuliko mwingine yeyote.

So guys chungeni sana na tumieni akili katika hili, mtu wako akija na kiherehere chake eti "fulani ananitaka" we muulize "umemjibu vipi". Hapo ndio utajua huyo kweli ni mtu sahihi ama la.

Na nyie kina dada kama sio makusudi ya kutimiza mambo yenu, unamkuta mtu ana uhusiano mzuri tu na rafiki zake pengine wamesoma toka secondary hadi chuo pamoja, then unaenda kusema hayo maneno unatarajia nini? Mnajua kabisa urafiki unakufa na ndio mnachotaka.

Wanaume wenzangu sisemi hivi kuwatetea marafiki ambao wana nia mbaya dhidi yako hapana bali wanawake pia huwa wana body language zao, manzi anaeza akakutizama tu ukajua anakutaka, sasa hawa wanawake wa namna hii ndio huwa wanaonyesha ishara hizi then masela wanashindwa kuvumilia, inabidi watose ndoano majini.

Mnaweza mkawa mpo kwenye party unakuta mwanamke wako anamrembulia mwamba huku we hujui kiendeleacho, after then jamaa anaona kumbe huyu manzi ni chama la wana anaona bora apite nae.

Ukikutana na mwanamke wa namna hii anza kuwa makini.

Take care guys, wanawake kuishi nao tutumieni akili nyingi.

Utahitalafiana hadi na mkoa mzima kwa wanawake wa type hii, serious

EDITED.
 
Nakumbuka back in the days 2009 huko kuna jamaa yangu alikuwa zaidi ya ndugu yangu....alikuwa ni mtu wa wanawake sana so alikuwa na demu wake mmoja ambaye kidogo walikuwa serious...
Sasa kila siku ugomvi mara akutwe na demu mwingine gheto nakuja kufuatwa mimi kusuruhisha.
Bhas visa vikawa vingi mno na jamaa akawa hajali sana siunajua wanaume tulivyo.
Kuna siku demu wake akanitumia text, anataka tuonane tuongee nikakubali tukaonana....
Katika maongezi demu anadai ananipenda mimi hampendi tena jamaa yake, nikajaribu kumuelekeza na kumuonesha kwamba anachofeel kwa muda ule sio mapenzi ni hasira so atulie tu na jamaa atarudi na maisha itakuwa kama zamani.
I had to respect my brother na sikutaka hata kumwambia nilitaka nisimfanye ajisikie vibaya....by the time nilikuwa na uwezo wa kumla yule demu n.k lakini sikutaka.

Kimbembe kilikuja walivopatana, demu akamjaza jamaa maneno eti mi nlikuwa namtongoza na alinikatalia...[emoji1]
Jamaa yangu alini-mind na ushkaji ukafa.

Baadae alikuja kujua ukweli akaniomba msamaha nlishamsamehe kitambo lakini ushkaji hauwezi kuwa kama zamani.

Kuna baadhi ya wanawake hawajielewi.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Pole sana mkuu, ni kweli ndio walivyo, huyo dada alijua one day utamwambia rafiki yako, so aka kuwahi akijua ataaminika.
Wanawake wana hizi tabia sana.
 
Ishu iko hivi;

-Mwanamke akikwambia flani ananitongoza jua hampendi huyo mtu wala hana mpango nae maana anajua utamkataza tu.

-Mwanamke anagongwaga kimya kimya tu na mtu anaempenda tena atafanya mbinu zote usijue.
Bro yamekukuta nini?
Mwanamke lazima atengeneze trust kwako kwamba yeye ana msimamo.
Then analiwa na huyo huyo,
 
Back
Top Bottom