Kuna mmoja alikuwa anamwambia boy wake wale majirani unaoendaga kuwasalimia (sisi) wamenisemea kwa Baba eti tumefanya mapenzi,,, boy alituwakia akaacha kuja hata kutusalimia bibie alifurahiii.
Ikaja boy anapenda kwenda duka flan hiv na muuzaji ni binti age ya 20 Hiv sa akifika pale atapiga story ndo arudi siku moja akamwambia boy wake yule wadukani kakataa kunihudumia ameniitia vijana wakawa wananisema kuhusu mapenzi yetu boy aliwakaaa akahama barabara kbs binti huyo binge la smile.
Sasa bhana alipopanga maji walikatiwa akawa anachota kwa Jirani km kawaida bombani wahudhuriaji wengi ni wakike boy kwa mastor wee bibie akampandia boy ooh wale wabombani wameniambia eti "mume wako peke yako akiwa ndani akiwa nje ni wa wote" .
Boy alijikuta anachukia mtaa wote hasa wanawake akamwambia bibie basi uwe unskuja kunichotea maji kunipikia ili Mimi nisiende maana wanatafta kutuachanisha,,,
Binti akaingia ulingoni anafanya kazi zote anarudi kwao, siku aliposikia boy anashoboka na majirani kwa Shangwe ndo aingie gheto kwake bibie akajipanga oooh nlikuwa nafua hao wapangaji wakanimwagia ndoo ya maji ya kuoshea vyombo eti wanasema sifai kuwa na wew
Ha hahah jamaaa hapa akili ndo ikamkaaa sawa coz wapangaji hao anawajua vizuri. ila ndo keshachelewa ivo.