Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,730
- 530
Samahani Mod, imenibidi niitenganishe hii mada ili kuwaomba wadau na hasa Mwanakijiji kupitia KHL wawatafute hawa wazee ili watoe mawazo yao kuhusu IOC kwa sababu zifuatazao:-
KAWAWA
Ni mpigania Uhuru pamoja na Nyerere na amefanya kazi na Nyerere kwa muda mrefu, pia ni Muislamu na alikuwa Waziri wakati Nyerere akifuta Mahakama ya Kadhi na kutaifisha Shule za Wakristo.
Wakati suala hili la OIC likiendelea, Mzee Kawawa amekaa kimya kabisa na hatujui msimamo wake ni upi katikahili akiwa kama Mzee aliyefanya kazi na Nyerer na kupitisha maazimio magumu pamoja naye.
MWINYI
Alikuwa Rais wa Tanzania na ni wakati wa utawala wake ndipo Waislamu walidhinikiza sana masuala ya Uislamu katika nchi yetu, pia amewahi kunukuliwa kusema kuwa Wakristo wasiohofu kuhusu Mahakama ya Kadhi maana itakuwa haihusiki na mabo ya Jinai.
Hata hivyo hatujawahi kusikia kauli yake kuhusu Tanzania kujiunga na OIC ingawa tunajua kuwa OIC na Mahakama ya Kadhi ni mapacha!
Ni wakati wa Utawala wake ndipo Zanzibar ilijiunga na OIC na ni ajabu kuwa 'alikuwa hajui' hilo na sina uhakika kama lilifanyika kwa kibali chake kama Rais wa Tanzania au la.
OMBI LANGU:
Waandishi mliomo humu muwatafute Wazee hawa ili Watanzania tusikie kauli na misimamo yao kuhusu masuala haya; kimya chao kinanipa wasiwasi maana kama Rais ameshituka juu ya mwelekeo wa majadiliano nao Wazee wetu wapo kimya maana yake nini?