Oil kupungua bila kuwa na leakage

Makobus

Senior Member
Joined
Jul 30, 2012
Posts
169
Reaction score
110
Habari ndugu zangu. Naomba mnisaidie kujua kwa nini ninapoendelea kupima oil ya engine kwa dipstick ninaona inapungua wakati hakuna mahali popote panapoonesha kuvuja (leakage) kwa oil hiyo. Inayopungua inakwenda wapi? Natanguliza shukrani.
 
Inatoka kama moshi, inaungua kwenye combustion chamber za engine yako, kafanye service ubadili gaskets, wataalam watakuja kukwambia, anyway ni injini gani hiyo na inapunguza oil kwa kiasi gani?
 
Nashukuru. Engine yangu ni 1NZ vvt-i. Niongezee nondo boss.
 
Hiyo engine ikianza kunywa oil ni bora kununua mswaki, itakusumbua siku zote kila baada ya mda mfupi.
 
Ushauri nifanye nini ili isifike pabaya?
 
Mswaki ni engine bila vitu kama compressor,starter
Mimi siyo mzoefu kabisa wa mambo ya magari. Naomba univumilie tu ninavyozidi kuuliza. Naomba unifafanulie kwa uwazi kabisa tofauti ya 1NZ vvt-i na hizi mswaki. Ahsante.
 
Hata ya kwangu ilikuwa ina shida kama hiyo, fundi akaniambia piston ring zitakuwa zimechoka hivyo tufanye engine overhaul, tukafanya mwaka jana mwezi wa 11, mpaka leo iko poa mpaka muda wa kumwaga oil ukifika oil inakuwa bado iko poa.
 
Hata 1NZ ina mswaki kwa maana unabadilisha injini nusu ikiwa haina baadhi ya vitu kama alivyovitaja hapo juu.
 
Hata ya kwangu ilikuwa ina shida kama hiyo, fundi akaniambia piston ring zitakuwa zimechoka hivyo tufanye engine overhaul, tukafanya mwaka jana mwezi wa 11, mpaka leo iko poa mpaka muda wa kumwaga oil ukifika oil inakuwa bado iko poa.
ulitumia kama sh ngapi,ufundi na vifaa
 
Mimi siyo mzoefu kabisa wa mambo ya magari. Naomba univumilie tu ninavyozidi kuuliza. Naomba unifafanulie kwa uwazi kabisa tofauti ya 1NZ vvt-i na hizi mswaki. Ahsante.
'Mswaki' maana yake ni block la injini bila ya kuwa na parts nyingine kama nozzles, coils, starter, compressor, n.k. Injini complete ni ile yenye kila kitu kama ilivyo yako kwenye gari.
 
miye ningekushauri kama gari unahistoria Yake ni yako mwenyewe unaitumia kuliko ukafunguo engine upige mswaki bora uwe unaendelea tuu kuongeza oil kama haitoi Moshi mweupe ule nyuma
 
Ahsante sana kiongozi. Ushauri mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…