Serikali na mamlaka zake inadai inaendelea kupambana na vitendo vya kuchakachua mafuta ya dizeli na petroli, lakini ufuatiliaji niliofanya unaashiria kuwa baadhi ya watendaji ndani ya serikali na mamlaka zinazotarajiwa kudhibiti vitendo hivyo wanafahamu wanaofanya uovu huo na pengine kuwasaidia kwa namna mbalimbali.
Kampuni ya kusafirisha na kuuza aina mbalimbali za mafuta, yaani dizeli, petroli, mafuta ya taa na mafuta ya ndege, Oil Com inasadikiwa kufanya uchakachuaji mafuta kabla haijayaingiza sokoni.
Mei 20, mwaka huu gari la kampuni hiyo Scania Na.T517AJM lenye tela Na. 687ACP lililoendeshwa na S. A. Mkude lilipakiwa lita 35,000 za dizeli katika depot ya kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam.
Gari hilo likaegeshwa ndani ya Yadi ya kampuni hiyo iliyopo Tabata Relini. Safari ya kupeleka mafuta hayo Ushirombo wilayani Bukombe ilianza Mei 21 mwaka huu, siku ya Ijumaa ambapo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Kampuni inayojenga barabara ya Ushirombo mpaka Lunzewe, ambayo imeingia mkataba wa kuuziwa mafuta na Oil Com.
Afisa wa kampuni ya ujenzi, Gasper Msuya, alipelekewa mafuta na nyaraka zinazohusika na mzigo huo na Mkude Jumatatu asubuhi. Baada ya kuchukua sampuli ya mafuta kutoka ndani ya gari hilo na kuondoka nayo, alirejea mchana na kumueleza Mkude kuwa hawezi kupokea mafuta hayo, yamechakachuliwa.
Dereva na gari vikatakiwa kupelekwa polisi Ushirombo. Dereva akaomba polisi ishirikiane na EWURA wachukue sampuli ya mafuta hayo ikafananishwe na yaliyo kwenye matanki ya mafuta yanayomilikiwa na Oil Com yaliyopo Kurasini Dar es Salaam ambapo mafuta hayo yalichukuliwa kwa maelezo kuwa, wakati yakipakiwa hata yeye aliingiwa na shaka kutokana na wepesi wake.
Tofauti na matarajio, wakati dereva huyo akiwa rumande, ofisi ya Oil Com Kahama iliagiza dereva akachukua gari hilo siku hiyo hiyo ya Jumatatu. Inasadikiwa ilipelekwa Kahama. Dereva alishikiliwa na polisi tokea Jumatatu hadi Ijumaa ambapo aliambiwa ajidhamini kwa leseni yake, akae eneo hilo la Ushirombo kwa siku chache, waliomshitaki wasipofika ili apelekwe mahakamani angeachiwa huru arudi Dar. Hakupelekwa mahakamani kwani walompeleka waliingia mitini.
Ufuatiliaji ukafanikisha kupatikana namba ya simu ya kiganjani ya afande aliyeshughulikia sakata hilo na jina lake kwa sasa linahifadhiwa, akaitwa na kuhojiwa:
Swali: Tunazo taarifa kwamba mmekamata mafuta yaliyochakachuliwa na dereva anayetuhumiwa kufanya kosa hilo, suala hilo limefikia wapi?
Jibu: Ni kweli suala hilo lilitokea, lakini siwezi kulizungumzia kwa kina, waulize wakubwa
Swali: Wakubwa wakina nani? Si ulilishughulikia wewe?
Jibu: Nakushauri umuulize mkuu wa upelelezi.
Ufuatiliaji ukafanikiwa kupata namba ya mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Bukombe, Leonard Paul, alipoulizwa baada ya kuelezwa sakata lote lilivyokuwa tokea gari lilivyopakia mzigo hadi lilivyofika mikononi mwa polisi Ushirombo alisema hivi:
"Kwakweli sina taarifa za uhakika za kukueleza kuhusu suala hilo. Kwanza tokea Mei 20 mpaka Mei 30 mwaka huu, sikuwepo wilayani nilikuwa mafunzoni mjini Morogoro. Hata sasa tunavyozungumza nipo vijijini kikazi, nikirudi wilayani nitafuatilia na kutoa ufafanuzi."
Kwa mwendo huu, mchezo huu mchafu utakwisha? Kwa vyovyote hizo lita 35,000 zilisambazwa sokoni baada ya kushtukiwa na kampuni ya ujenzi na kutolewa nje, yalipelekwa wapi? Hilo ni swali linalohitaji kufanyiwa kazi...