SoC01 Okoa Mazingira, Safisha Miji na Kujipatia Kipato

SoC01 Okoa Mazingira, Safisha Miji na Kujipatia Kipato

Stories of Change - 2021 Competition

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Tatizo (Problem worth Solving)
Nishati ni muhimu sana kwa jamii ya sasa, kwa bahati mbaya sana tunatupa nishati hiyo kwa kuharibu mazingira badala ya kuitumia na kuendelea mzunguko (Life Cycle)…,
YAANI... (Tunachafua Huku).....
1626684479418.png

Na Kuharibu Hapa.....
1626684515792.png

Ili Tupate Hiki....
1626684548452.png

Wakati tungeweza kupata hicho (Nishati), Kwa kutumia ule tunachoita uchafu (Mabaki), na kupata mbolea ya kuendeleza kile tunachoharibu (Mimea / Misitu / Mazao)…

Yaani….

Waste – Biogas – Fertilizer

Ushauri (Solution)
Ushauri ni kuwatumia wadau wafuatao:-
  • Magereza (ambao wanatumia sana kuni kwa kupikia na wana uhitaji mkubwa wa nishati ya kupikia
  • Mashule yote ya boarding au yale yanayohitaji nishati kwa kupikia
  • Wazalishaji taka wote (masoko, migahawa, mahoteli) n.k.

Ufanyaji kazi (Mode of Operation)

Magereza

  1. Kupiga marufuku matumizi ya kuni kwa magereza zote na mbadala wake kutengeneza Biogas plant;
  2. Ili kuilisha hio Biogas plant Magereza watakuwa wanapita na magari yao (au wakipigiwa simu kama kuna taka nyingi sehemu Fulani mfano sokoni ili wazifuate. Kwa wale wadau wote wazalisha taka magereza itawapa sehemu ya kuwekea taka ambapo inabidi watupe kulingana na aina ya taka pia waweke (biodegradable peke yake). Pia kwa Magereza kama Butimba Mwanza kuna Source nyingine kubwa ambayo ni hatari kwa mazingira (Magugu Maji) ambayo hatari yake kwa mazingira na viumbe hai majini ni kubwa sana.
  3. Kupata Gesi kwa haraka mchanganyiko wa taka na samadi ya ngo’mbe inasaidia zaidi hivyo basi Magereza wanaweza wakawa na ngo’mbe wachache ambao watakuwa wanawalisha magugu maji na mabingo (Elephant Grass) - (majani ambayo yanakuwa kwa kasi sana) na mbolea inayotoka kwenye hio Biogas inaweza kusaidia kukua kwake.
1626687330612.png
Hivyo basi magereza pamoja na kuwa na Biogas plant inaweza pia ikawa inafuga ngo’mbe kadhaa kwa ajili ya kuchanganyia mabaki / taka

Mashule / Mahospitali / Migahawa (Watumiaji Wakubwa wa Nishati kwa Kupikia)
Magereza iwasaidie hawa wadau kutengeneza Biogas Plant, katika mazingira yao ila management ibakie kwa Magereza kila siku magereza kwa kutumia magari yao wanaweza wakawa wanapita na kuzifeed hizo Biogas kwenye mazingira ya wateja wao na kuchukua mbolea (feeding and emptying) kwa kufanya hivyo hii itasaidia kwa watumiaji kupata nishati kwa bei rahisi kuliko vinginevyo na magereza kupata mbolea, vilevile faida kwa jamii itakuwa ni utunzaji wa Mazingira

Faida kwa Magereza
Zaidi ya kutunza mazingira na kusafisha miji, masoko, vyanzo vya maji (kuondoa magugu maji), mabaki / uchafu kutoka kwa wafugaji n.k. kwa magereza kuzunguka na kukusanya mabaki hayo, na kupunguza hewa ukaa, pia magereza itapata faida zifuazo:-
  • Kuchaji pesa kidogo kwa kuwaondolea uchafu wazalishaji wa uchafu, (masoko, migahawa, wafugaji, manispaa maofisi n.k.) Ikumbukwe hata karatasi inaweza kuwekwa kwenye biogas plant.
  • Kuchaji pesa kwa kusaidia kutengeneza na kuwapa feedstock kila siku (mashule, migahawa na wahitaji wa nishati ya kupikia kwa wingi)
  • Kuuza mbolea inayopatikana
  • Kufuga ngo’mbe jambo ambalo litawasaidia katika kuchanganya feedstock pamoja na mabaki mengine. (optional)

Faida kwa Jamii
  • Kuokoa Mazingira na kupunguza uchafu mitaani na mijini na kupunguza uchafu wa kupelekwa dampo,
  • Kuwekewa sehemu za kutupa taka tofauti tofauti (maintained by magereza)

Faida kwa Mashule / Migahawa na watumiaji wakubwa wa Nishati kwa Kupikia
Kupata nishati kwa bei nafuu, kwa kujengewa Biogas na Magereza na kuletewa feedstock kila siku na kusafishiwa hio Biogas (full maintenance)

Mahitaji kwa Magereza
  • Magari ya kukusanya taka, na kusambazia feedstock kwa wateja wake.
  • Biogas Plant kubwa kwenye eneo lao ili wapate gesi ya kupikia na pia kusaidia kutengenezea mashule na watumiaji wakubwa biogas plants (kwenye maeneo yao)
  • Ufugaji wa ngombe wachache (optional)
  • Shamba la bingo bingo (Elephant Grass) kulishia ngo’mbe (optional)
  • Workforce (Wafungwa)
Hitimisho;
Kwa kufanya hayo juu tutapata yafuatayo:-
  • Kupunguza ukataji miti kwa ajili ya kuni
  • Kusafisha miji yetu
  • Kuongeza recycling ya taka ambazo zinapelekwa dampo na kuwa kero kwa jamii husika ya sehemu hizo
  • Kuongeza upatikanaji wa Mbolea
  • Kutumia nguvu kazi iliyopo (wafungwa) kusafisha miji yetu
  • Kusaidia kupunguza tatizo la magugu maji kwenye Ziwa Victoria
  • Magereza kusaidia kuweka sehemu za kutupa taka kwa wazalishaji taka wakubwa na sehemu zenye watu wengi (hapa wanaweza kuweka Security Camera kuhakikisha watu wanatupa uchafu tofauti sehemu tofauti kama ilivyoolekezwa (bila plastic au vitu visivyooza) Au Sehemu kama Sokoni kuwa na Mlinzi (Mfungwa) kuhakikisha taka hazichanganywi na visivyotakiwa.

NB:
Unaweza kuuliza hapo Napata vipi Kipato mbona kama Magereza ndio wanufaika wa kipato ? Jibu ni kama ifuatavyo:-
  • Watumiaji wakubwa wa Nishati kwa kupikia kupunguza gharama za matumizi (Money Saved is Money Earned) (Mashule, Migahawa n.k.)
  • Mazingira kuwa Masafi itapunguza gharama za Magonjwa kwako, na gharama kwa manispaa husika katika usafi hivyo pesa hio kutumika pengine.
  • Upatikanaji wa mbolea hivyo kusaidia wakulima na kuongeza mazao jambo ambalo litaongeza tija katika mazao hivyo wote kunufaika
  • Outlet nyingine ya kuondoa taka zako (unaingia mkataba na magereza wapite kuchukua) kwa gharama ndogo kuliko kawaida.
 
Upvote 2
C. C. Waione Magereza;

Zawadi kutoka kwa KeyserSoze AKA the The Solitary Socialist....
 
Back
Top Bottom