Okwi aidai Yanga zaidi ya 107 milioni

Okwi aidai Yanga zaidi ya 107 milioni

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Okwi amepeleka malalamiko TFF ya kuidai Yanga USD 62,000 [zaidi ya 107m].
Mchangunuo wa huo mkwanja ni kuwa hakulipwa USD 50,000 ambazo ni ada ya usajili na USD 12,000 ambazo ni kama mshahara ambao hakulipwa.
Amewapa dedline mpaka 15/02/2015. Amedai wakigoma kumlipa, mahakama itafanya kazi yake. Nakala imepelekwa kwa Mhindi pamoja na FIFA.

NB: Eeeh Mungu saidia huyu mja wako apate haki yake.
 
Ingekuwa inawezekana Okwi angezuiwa kucheza soka hapa Tanzania
 
Ingekuwa inawezekana Okwi angezuiwa kucheza soka hapa Tanzania

Tunatakiwa tushukuru kua na Okwi mda huu, maana anawapa somo kubwa viongozi wetu.
Next time watakua makini wanaposaini mikataba.
 
Nimeipenda "nakala imepelekwa kwa Mhindi ......"!
 
Na hasira za kutolewa Mapinduzi Cup na JKU jana sijui kama watamlipa.
 
Hapo anavuta kasi baadaye atawadai Simba ndio maana kagoma kurudi. Sisi tutamlipa za Kaseja maana ni nyingi kuliko anazotudai sisi, ninyi je?

tutamlipa za etoil du sahel.
 
Hapo anavuta kasi baadaye atawadai Simba ndio maana kagoma kurudi.
Tayari yuko Zanzibar pamoja na Ivo isipokuwa Owino ndo bado hajafika huko, sababu yake ni kuanzia benchi baadhi ya mechi, hawa wachezaji sijui kwa nini wana ubinafsi hivyo, timu ina wachezaji zaidi ya 25 na wanaoanza ni 11 tu sijui kwa nini kuna wengine wanaona wana haki ya kuanza tu kila siku na kama ni hivyo basi kuna sababu gani ya kuwa na wachezaji 25 au 30? Hata mwanaSimba mwenzetu Kaseja naye kama alisusa kwa sababu hiyo huo mimi nauita ni ubinafsi.
 
Kumbe Okwi yupo unguja? Sioni ni kwa jinsi gani Polisi watashinda leo.
 
Kumbe Okwi yupo unguja? Sioni ni kwa jinsi gani Polisi watashinda leo.

Leo anaweza asicheze maana alifika huko jana na sina hakika kama alifanya mazoezi na wenzake.
 
Back
Top Bottom