Okwi awashangaa viongozi Simba SC kushindwa kusajili hadi sasa

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253
Mshambuliaji wa Simba raia wa Uganda, Emmanuel Okwi, ameshangazwa na uongozi wa timu yake kwa kushindwa kusajili mchezaji yeyote mpya mpaka sasa.

Okwi amesema siku za usajili zimebaki nne kabla dirisha dogo la usajili kufungwa na anashangazwa kuona mambo yapo kimya.

“Nimepata hofu baada ya kuona siku zinakwenda halafu hakuna usajili wowote ambao tumeufanya wakati wapinzani wetu kwenye mbio za ubingwa Yanga na Azam FC wamesha sajili wachezaji watatu Hadi wawili,” alisema Okwi.

Mshambuliaji huyo amesema kama wanashindwa kusajili anahofia mambo kuzidi kuwawia magumu na hata kushindwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu kwani ushindani umekuwa mkubwa tofauti na matarajio yao wakati wanaanza msimu.

Awali kulikua na tetesi kuwa klabu hiyo itamsajili beki na nahodha wa Lipuli FC Asante Kwasi lakini inaonekana tofauti kwani Hadi sasa mambo yapo kimya .

Simba imepanga kuongeza wachezaji wanne kwenye dirisha dogo wachezaji hao ni kipa mmoja beki wa Kati mmoja na beki wa pembeni mmoja na mshambuliaji mmoja.
 
Angepeleka maoni yake moja kwa moja kwa uongozi wake ingependeza zaidi
 
usajili wa simba huwa ni pasua kichwa mpaka okwi mwenyewe ameona lakini viongozi hawaoni. ukiangalia gyan na mavugo walioletwa kumaliza tatizo la ushambuliaji simba wote hao ni mawinga. lakini kamati ya usajili mpaka leo inaamini kuwa mavugo na gyan ni washambuliaji wa kati. mbaya zaidi hata makocha nao wanawatumia kama washambuliaji wa kati. kwa anayeufahamu vizuri mpira angewatumia kama mawinga na ubora wao ungeonekana. sasa hivi simba inatakiwa itafute washambuliaji wawili wakati wa kumpa changamoto boco na iachane na luizio au imtoe kwa mkopo kwa sababu luizio toka ametoka kwenye majeraha hajapata muda mrefu wa kucheza ili kurudisha kiwango chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…