Okwi kukosa mechi na Lipuli leo

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,696
Reaction score
2,253


Hiki hapa kikosi kitakachoshuka dimbani kuikabili Lipuli

Mshambuliaji wa klabu ya Simba Mganda Emmanuel Okwi hajajumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachovaana na Lipuli FC kwenye mchezo wa ligi kuu leo jioni.

Okwi ambaye ni majeruhi alidhaniwa kurejea leo kutokana na ujumbe wake ambao aliutoa katikati ya juma, ukiashiria kuwa ameshapona lakini huenda kocha Joseph Omog ameamua kuendelea kumpa mapumziko ili arejee vyema.

Kikosi kamili cha Simba kilichotajwa leo kwaajili ya kuvaana na Lipuli FC kinaundwa na kipa Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein, Mlipili na James Kotei. Viungo ni Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Mwinyi Kazimoto na Haruna Niyonzima. Washambuliaji ni Shiza Kichuya na John Bocco.

Kwenye benchi wapo Mseja, Laudit Mavugo, Ally Shomari, Juma Luizio, Mwambeleko, Mwanjali na Nicolas Gyan.

Simba ipo kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 22 sawa na azam FC yenye alama 22 zikitofautina idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa. Lipuli ipo nafasi ya 7 ikiwa na alama 13.

EATV
 
Mbona habari sijaielewa Mara okwi Mara Ndikumana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…