Okwi na Aishi Manula kuikosa Lipuli,wakiisubiri Yanga

Okwi na Aishi Manula kuikosa Lipuli,wakiisubiri Yanga

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
Zikiwa zimesalia siku tisa kuelekea mchezo wa watani wa jadi, wachezaji tegemeo wa kikosi cha kwanza cha Simba mshambuliaji, Emmanuel Okwi na kipa, Aishi Manula, wanahatihati ya kucheza mechi ya kesho dhidi ya Lipuli ili kuepuka kuikosa Yanga.

Simba na Yanga ambazo zote zinadhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, zinatarajiwa kukutaka katika mechi ya marudiano ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayofanyika Aprili 29, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.

Okwi ambaye ndiye mshambuliaji anayeongoza kwa kupachika mabao, ameshatikisa nyavu za wapinzani mara 19 na Manula 'Tanzania One' wote wana kadi mbili za njano na endapo wakipata kadi nyingine katika mechi dhidi ya Lipuli kesho, rasmi wataikosa Yanga.

"Taarifa za kadi zote tunazo na wahusika hasa benchi la ufundi ndio wataamua nini kifanyike katika mechi ya Jumamosi huko Iringa," alisema kwa kifupi Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji 'De la boss' Manara.

Alisema pia benchi lao la ufundi lina taarifa kuwa kiungo wao, Jonas Mkude, hataweza kucheza katika mechi ya Lipuli, hivyo anaamini tayari watakuwa wanajua mbadala wake na kuhakikisha ushindi unapatikana na kuendelea na vita ya kuwania ubingwa.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, lakini Simba ndio timu pekee mpaka jana ilikuwa haijapoteza pointi msimu huu.

Mechi hiyo ya watani wa jadi inatarajiwa pia kutoa picha halisi ya mwelekeo wa kuwania ubingwa huku timu zote mbili zikiwa zimeshatolewa katika mashindano ya Kombe la FA ambayo bingwa wake atapata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika hapo mwakani.

Kwa maana hiyo, timu moja kati ya hizo kongwe, mwakani haitashiriki mashindano yoyote ya kimataifa na sababu hiyo inaongeza ushindani kwenye mechi zao zote za ligi zilizobakia wakati huu Simba ikiwa kileleni kwa pointi 58, ikiwa ni 12 mbele ya Yanga yenye mechi tatu mkononi.
 
Yanga tunajiandaa kucheza na TP Mazembe, Enyimba.El Masry, mechi za kipuuzi kama hiyo ya Simba hatuna habari nayo...Sisi tuko kimataifa zaidi
 
Umeumbuka mkuu usipende kutunga habari au kucopy na kupaste. Hakiki chanzo cha habari kwanza.
 
Back
Top Bottom