Okwi anatarajia kutua nchini kesho Jumamosi na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe maarufu kama ZHP amethibitisha.
Hans Poppe amewaambia waandishi wa habari leo kwamba Okwi anakuja kumalizana na Simba na kazi itakuwa ni kusaini.
“Anakuja Jumamosi, hapa ni suala la kusaini kwa kuwa suala la mazungumzo tulimaliza Kampala,” alisema Hans Poppe.