Huelewi nini??? Hao ni vijana wa zamani kama mimi wakikumbuka enzi zile za miaka ya mwishoni 1980 na mwanzoni 1990. Wakti huo redio stesheni ilikuwa ni rtd (sasa tbc).Wakti nyimbo hizi zinatamba, rutashubanyuma ulikuwa hata mimba yako kutungwa bado ndo maana unaona ni kitu cha ajabu (NB: JOKES). Mie binafsi nkisikiliza nyimbo hizi wakti huu huwa nakumbuka maisha ya shule ya msingi.
Kama kuna mdau ana nyimbo hizi; halima, bomu la simanzi, pendo na kisa cha mesenja zilizoimbwa na bima lee naomba aniwekee hapa. Na pia ule wimbo wa uhuru wa zimbabwe wa ddc naomba kama kuna mtu anao auweke.