Ole Naiko: Mnatuonea watu wa Monduli

Kwa mujibu wa kanuni na uendeshaji wa TIC kama inavyoonyeshwa kwenye tovuti yake, wao TIC ndio hutafuta leceni, mambo ya ushuru na forodha na kadhalika kwa niaba ya wawekezaji.

Ikiwa Naiko anadai RDC walikwenda kwake wakiwa wamesajiliwa BRELA na wana kibali cha TRA, je hii kampuni ilisajiliwa Tanzania kama makao makuu? kama ni kampuni ya nje ya uwekezaji, ilikuwaje wakaacha kwenda TIC na kukimbila kwingine kote kisha warudi TIC?

He is trying to fry himself! JF tuna kuni, kiberiti na mafuta atuambie ni saa ngapi tuanze kumkaanga!


http://www.tic.co.tz/

 
Huyu jamaa is on his way out period. He knew very well that he was out the door before the Richmond saga. He cannot perform. Anything else said would be a lie.
 
Mkabila utamjua tu,kwa matendo!yeye angejitetea bila ya kusema maneno kama haya.Viongozi wetu wa Dini wa siku hizi bwana.wamekaa kibiashara sana.Mungu atuepushie Mbali.Huyu Asikofu Laizer ni Mpuuzi na Mla Rushwa tu!anatetea mtu Mfisadi ili khali anjua ufisadi ni dhambi!

Lowassa kama Mwinyi?mwenye kitabu cha Uongozi na Hatma ya Tanzania,naomba aweke copy yake hapa.
 

Sijakuelewa ndugu PM,
Kwamba unakubaliana na Ole Naiko kwamba kamati ya Mwakyembe ilikuwa inatafuta visa na watu wa Monduli? Kamati ilikuwa na kazi ya kutafuta ukweli kuhusu uhalali wa Ricmond, na sio uwepo wa watu wa Monduli mahali fulani. Huyu jamaa anapindisha ukweli wa mambo. Lazima tumuwashie moto tu!
 
Ole Naiko, Ole Naiko!

Aache kuongea kauli ambazo hazina mwelekeo.

Naona huu mkakati wa kujisafisha ni wa kiwango cha chini kupita maelezo. Ole Naiko alikua wapi siku zote asiyasema haya ya sasa? Kwa nini hadi EL alipoanza kutaka kujisafisha ndipo na yeye anafuata? Angeongea haya mara baada ya ripoti ya bunge ningeelewa kidoooogo.

Kuna mtu amemwambia kwamba wamasai wanachukiwa Tanzania? Uweo wake wa kufikiri una ukomo gani? Au anataka kutueleza kwamba EL alihusika kumfanya yeye mkurugenzi wa TIC?

Sasa hivi Severe naye anawweza kuibuka na kudai kwamba kuondolewa Maliasili ni ukabila!
 
EL ni Mmeru kabisa kama anabisha aje hapa jf kupinga halafu aone wamasai wa kweli watakavyomjibu kwa ushahidi.wewe ole naiko funga mdomo wako mana unajitafutia balaa na ukabila hapa haupo
 
Mimi ninaona kwa kauli zake za Utetezi kuzihusisha na Ukabila bila Udhibitisho wowote , basi amejifukuzisha kazi.kwa sababu TIC kama institution haina kabila, wapo wazaramo/ngoni/masai etc.
Yeye angejitetea au angitetea TIC kwa Facts , sio kuegemea ngao ya ukabila.
Hizo Facts ulizo ziweka wewe angeweza kuzitumia kuitetea TIC.
Maana tanzania tunashudia alot investor wanakuja na brief cases tu, badala ya tangible things which can denote that person to be a real investor.
one ni detail profile ya Directors, Pili Uwezo wa Kifedha, Wataalamu aliokuwa nao ambo zitakwenda na Sheria zetu za kuajiri Tx, tax clearance anakotoka,Published Accounts ikiwezekana Past 5 years etc
La Pili ndugu yangu ni ikiwa kila mtu atajitetea kwa ukabila/udini wake , kweli patakali hapa, maana Harrison alisema kuna watu walifikiri ni vita dhidi ya uislamu maana Msabaha alihusika na Karamagi, mara ikawa dhidi ya Lowasa and his cronies. Sasa Kesho kutwa sijui itakuwa Mnyakyusa ndio analia au mpare/Msukuma au Mchaga etc.
Ndio maana kuja nahaja ya ku-reform taratibu zetu za Ajira na uteuzi ili kuepuka upuuzi kama huu
 
Huyu bwana anaona anataka kuleta kitu kingine kiitwacho Ukabila ili kukwepa kutoka kwenye kashfa hii ni pia kumtetea bwana EL. Hawezi kutupeleka kwenye ukabila kirahisi hivyo .....TIC haiwezi kukwepa lawama hapa kama Richmond imejulikana kuwa ni kampuni hewa!!
 
Heshima mbele......Duh, hapo kwenye hiyo posti ya Rev kwa kweli na nimeenda kwa site mambo ni mambo.... Msinishangae nikisema kuna uwezekano wakuu wenye kuitwa "WATEKELEZAJI" hawajui function zao kabisaaaa... Nimesoma maelezo na kujitetea kwa Bin Naiko kwenye Thisday leo na kwa kweli nimeshituka sana kuona jinsi wanavyojitangaza na jinsi anavyojitetea!!!

Eee Molla Uibariki Tanzania yetu!!!! Kweli JK ana kaaaz kweli kweli kutimiza azma yake ya maendeleo na "Maisha bora kwa kila mTz" manake kama ni watendaji kweli amekosa!!!!!

By the way, nadhani huyo mheshimiwa aliongea on his own behalf and NOT waMaasai.... Sikumbuki siku alichaguliwa rasmi kuwa Laiboni wetu popote na hivyo alichokisema ni kama yeye na SIO kwa niaba ya Maasai "Maa"........ Mimi sina shida huku kijiweni kwangu ninapiga mzigo kama kawa na hakuna anayentenga na kunipiga vijembe!!!
 
Tehe tehe! Vijindoano vya kamati bado zawachoma choma, tehehehe, tapatapa tapatapa za vijidagaa navyo!. Silence should have been his best option!

Hao waandishi tehehehe🙄, ngoja niwaulize....Mliuliza nini?

Otherwise ole wenu naye yiko kwenye "RICHMONDULI"😀 tehe heh

Huu ukabila wa wapi? "RICHMONDULI"?

Give me a Break! au kwa lugha yangu...
 
"...And in his eight-page statement to the media, Ole Naiko stated that he was placing his fate firmly in God’s hands.

The TIC chief’s unexpected remarks came against the background of what is increasingly looking like a carefully-orchestrated campaign to try and clear Lowassa of any wrongdoing after the Richmond fall-out.

Various newspapers have begun churning out articles on literally a daily basis, singularly praising the ex-premier’s ’’courage and wisdom’’ in resigning over the Richmond corruption scandal and criticising the findings of the Mwakyembe committee."


This Day, 26 Feb, 2008.

This is it, my people.
 
 
 
Wakati mwingine unaweza kujiuliza kama kweli maoni ya Naiko yanaendana na nanafasi yake, amekwepa hoja na hivyo inaonesha kuwa kichwa chake hakukipa kazi.

Wanakamati ya bunge hawakumuhoji yeye kama mtu wa Monduli bali ofisa anayeshughulukia umma na usalama wake(upande wa uwekezaji)
Namshauri kuwa bado ana nafasi ya kutueleza ukweli na sio mambo ya umonduli hapa
 
"In a somewhat surprise move, Ole Naiko yesterday compared what he described as ’attacks’ on senior government officials who hail from Monduli District, Arusha Region - including Lowassa and himself - to ’’ethnic cleansing.’’

’’There is a danger of fomenting hatred against people who come from Monduli, and this can lead to ethnic cleansing,’’ the TIC boss told a news conference at the Centre's offices in Dar es Salaam."


ETHNIC CLEANSING??? NOT EVEN THE KENYAN CRISIS CAN BE TERMED ETHNIC CLEANSING!

HUYU OLE NAIKO AMELITIA AIBU TAIFA, YEYE MWENYEWE NA WATANZANIA WOTE KWA UTETEZI WAKE WA KIJINGA...NA WAHENGA WALISEMA, UKITAKA KUMUONA MWANAUME WA SHOKA, MSUBIRI UMWANGALI WAKATI WA MATATIZO ANASISIMAMAJE...YEYE NA EL WAMEDHIHIRISHA NI WABABAIKAJI YANAPOTOKEA MATATIZO, NA HIVYO HAWAFAI KUONGOZA JAMII YETU.
 
Lowasa ni kama mfamaji hutapatapa.Hata kukipita nyasi kwenye mawimbi basi hushikilia hizo nyasi kwa nia ya kwamba zitamuokoa.
Hata akisafisha namna gani hatakuwa safi daima kisiasa kwani atakuwa na madowa tu.Kwa Kiswahili halisi tunasema LOWASA NI MCHAFU KOGA.

Kamati teule ya Bunge kuhusu saga la Richmond haliwania kupiga ngwara mbunge wa Monduli wala wa Bagamoyo na wala wa Tanga. Ndugu Mwapachu pia kajiuzulu mwenyewe alipoona mambo yamemshinda na ujambazi unaendelea.
Sasa huyu anaesema Mbunge wa Monduli ndio alikuwa ni “Bangusilo” je watu wa Tanga watasema kwamba ndugu Mwapachu pia ni kafara la tume teule?

Wacheni mambo ya upuuzi na kusingizia vitu. Lowasa amefanya makosa yake na kuiweka nchi gizani kwa hiyo ilikuwa ni lazima awajibike.
UKIVULIA NGUO MAJI LAZIMA UOGELEE. Lowasa amefanya kama vile ilivyotakiwa, ameogelea.
Iliyobakia ni kumpeleka mahakamani akadadiswe vizuri ili arudishe zile fedha alizopewa na wakuu wa Richmond kama “BAHSHISH” kama zi hiyo “RUSHWA” halisi. Sasa hivi serikali inalipa Richmond 152m/- kwa siku wakati wanachi wake hawawezi kupata kutumia dola moja kwa matumizi ya kawaida.

Je Lowasa anapaswa kulipwa “pension” kwa uhalifu wote huu alioufanya? Katiba yetu inasemaje kuhusu hali hii? Au katiba inataka marekebisho ili mafisadi kama hawa wasipewe pension?
Sasa kama ni “Ethnic cleansing” itabidi AU ilete majeshi ili kulinda watu wa Monduli! Watu wanaropoka maneno tu! WENDA WAZIMU HAWA. Kweli mtu utamkinga mfisadi kwa kwa vile anatoka Monduli , Tanga, Bagamoyo au Arusha na kadhalika.

Ole Bakari Muhogo! (Picha sina ningelikuwekea hapa).
 
 
Mimi swali langu ni kama Kampuni iliyoomba kibali ni Richmond Tanzania Limited na iliyopewa mkataba kwa mujibu wa kibali hicho ni Richmond Development Company LLC, je wao TIC walifanya nini kuwaambia serikali kuwa kampuni mliyoipa mkataba au inayowekeza siyo iliyopewa kibali?
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…