Ole sendeka aongozewa mashitaka!

Mwikimbi

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2008
Posts
1,762
Reaction score
829
Ole Sendeka aongezewa mashitaka
Monday, 20 April 2009 16:49

Na Glory Mhiliwa, Arusha
KESI inayomkabili Mbunge wa Simanjiro (CCM), Bw. Christopher Ole Sendeka ambaye anashitakiwa kwa kumpiga Mwenyekiti wa vijana wa CCM Mkoa wa Arusha, Bw. James Milya imeendelea kunguruma jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ambapo mwendesha mashtaka wa Serikali ameongeza mashitaka ya kutishia kwa bastola.
Akisoma mashitaka hayo, Mwendesha Mashtaka, Bw. Agustine Komba aliiambia mahakama mbele ya Hakimu Mkazi Bw. James Karayemaha kuwa yameongezwa mashitaka mengine ambayo awali hayakuwepo.

Alidai kuwa Ole Sendeka anatuhumiwa Januari 9 mwaka huu wilayani Monduli katika semina ya wazee wa kimasai ambayo iliandaliwa na Mbunge wa Mbulu, Bw. Edward Lowassa alimtishia kwa bastola na kumdhuru mwili Bw. Milya.

Hata hivyo Mwendesha mashtaka huyo aliiomba mahakama kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza kesi hiyo ambayo imeshatajwa kwa mara mbili baada ya upelelezi kukamilika.

"Mheshimiwa hakimu naomba tarehe kwa ajili ya kuanza kusikilizwa na kutolewa ushahidi ambapo upande wa upelelezi umeshakamilika. Tutaleta mashahidi 13, bastola iliyotumiwa na mshitakiwa kutishia, fomu namba tatu aliyotibiwa nayo mlalamikaji," alisema Mwendesha Mashtaka.

Aliwataja mashahidi watakaotoa ushahidi kuanzia Mei 27 kuwa ni askari polisi wawili ambamo pia atakuwepo Mkuu wa Mkoa wa Singida, Bw Vicent Kone ambapo siku ya tukio alikuwepo kwenye semina hiyo.

Hakimu Karayemaha aliahirisha kesi hiyo mpaka Mei 27 ambapo itaanza kusikilizwa.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo. Mbunge huyo aliwashukuru wananchi wa jimbo lake waliojitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujua hatma ya kesi yake ambapo aliwataka kuendelea na kazi za ujenzi wa Taifa kwa vile sheria itachukua mkondo wake.

"Nawashukuru sana naona ni vyema wakulima muendelee na kilimo na wafugaji muendelee na ufugaji. Msihangaike kuja mahakamani tuache sheria ichukue mkondo wake," alisema Sendeka.





Powered by Business Times Limited
 
Nadhani hapa kuna kitu kikubwa zaidi.. Halafu Mkuu wa Mkoa wa Singida.. halafu nikikumbuka aliyoyasema Bungeni..

I don't know.. kila kitu kwangu mimi sasa nashuku tu!
 
Huyu mkuu wa mkoa ndio yule ambaye anatajwa kuhusika na mgogoro wa Kijiji cha Kisasida kinachogombewa na Kampuni ya Rostam na yakina Mwakyembe kwa ajili ya kuzalisha umeme wa upepo? Kama ndiye basi mambo!
 
For sure wanataka kummaliza. Huko ni kutaka kulipiza kisasi. Kuna siri kubwa hapo??Edo=RA=Rich wa Monduli=Olesendeka(Mabomu ya Ufisadi, pendekeza kuundwa kwa kamati ya kuchunguzwa Rich wa monduli, .....n). Je kwa mtindo huu tutafika??
 

Hivi baada ya uhamisho wa ma-DC na ma-RC kuna uhamisho mwingine wa wabunge kwenda kwenye majimbo mapya???
 
Hivi baada ya uhamisho wa ma-DC na ma-RC kuna uhamisho mwingine wa wabunge kwenda kwenye majimbo mapya???

...Nikipata ajira kumshauri muungwana (verry soon nitateuliwa)
hii ndo itakuwa task yangu ya kwanza kushauri kuhamisha wabunge majimbo (wa ccm) na wengine kuwapiga chini hasa wale wenye kidomodomo sana. hehehe very interesting.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…