Pre GE2025 Olengurumwa ataka mjadala wa Kitaifa kabla ya kugawa majimbo ya Kiuchaguzi

Pre GE2025 Olengurumwa ataka mjadala wa Kitaifa kabla ya kugawa majimbo ya Kiuchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, ameiomba Time Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kufanya mjadala wa Kitaifa na wadau mbalimbali wa demokrasia juu ya mchakato wa ugawaji wa Majimbo ya Kiuchaguzi kabla ya mgawanyo huo kufanyika, ili kufanya maboresho ya kugawanya majimbo hayo.

Akizungumza Machi 12,2025 Jijini Dar es salaam, Olengurumwa amesema mchakato huo upo kikatiba ambapo Tume Imepewa mamlaka ya kufanya uchaguzi na ukaguzi wa majimbo kila baada ya miaka 10, ambapo kwa mwaka 2015 majimbo 26 yaliongezwa miongoni mwa majimbo yaliyokuwepo kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa ambavyo ni Idadi ya watu na Jiografia ya majimbo.

Olengurumwa amesema kabla ya Serikali kufanya mchakato huo kwa mwaka huu, ni vyema INEC wakawashirikisha wadau wengine ili kufanya maboresho zaidi juu ya ugawaji wa majimbo hayo kwani vigezo vinavyotumika havitendi haki kwa maeneo mengine.

"Kuna mikoa ina majimbo mengi lakini ukiangalia idadi ya watu ni ndogo sana na ukiangalia jiografia yake ni ndogo, na kuna mikoa ina majimbo machache ila ina watu wengi mfano mkoa wa Arusha una watu zaidi ya milioni 2.5 lakini kijiografia ni mkubwa sana na mjimbo ni machache sawa na Njombe na kwingine.
Lakini kuna maeneo kama Zanzibar ina eneo dogo lakini kuna majimbo 50."

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Sambamba na hilo wakili Olengurumwa ameongeza kuwa, Wilaya ya Ngorongoro iliyopo Arusha ambayo kijiografia ni kubwa sana kwani Inakadiriwa kuwa na Mita za mraba 14,000 ambapo Mkoa wa Dar es salaam unaingia karibu mara 10 lakini ina jimbo moja ambalo lina muwakilishi mmoja, jambo linaloweka mazingira magumu kwa wakazi wa jimbo hilo kwenye hatua za kimaendeleo kwani hata mbunge wa eneo jimbo hilo akifanya ziara kwa kata zote, itachukua muda mrefu kulimaliza eneo lote hivyo kulazimika kutumia rasimali nyingi zinazoweza kupunguzwa endapo majimbo yataongezwa.

Olengurumwa amesema inatakiwa kufanyika tathmini kubwa ya Ugawaji wa majimbo kwani vitu vya msingi vikizingatiwa kwenye mchakato inaweza kupunguza idadi ya majimbo hayo badala ya kuongeza jambo linaloweza kupunguza gharama za uendeshaji.

Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa, ameiomba Time Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kufanya mjadala wa Kitaifa na wadau mbalimbali wa demokrasia juu ya mchakato wa ugawaji wa Majimbo ya Kiuchaguzi kabla ya mgawanyo huo kufanyika, ili kufanya maboresho ya kugawanya majimbo hayo.

Akizungumza leo Machi 12,2025 Jijini Dar es salaam, Olengurumwa amesema mchakato huo upo kikatiba ambapo Tume Imepewa mamlaka ya kufanya uchaguzi na ukaguzi wa majimbo kila baada ya miaka 10, ambapo kwa mwaka 2015 majimbo 26 yaliongezwa miongoni mwa majimbo yaliyokuwepo kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa ambavyo ni Idadi ya watu na Jiografia ya majimbo.

Olengurumwa amesema kabla ya Serikali kufanya mchakato huo kwa mwaka huu, ni vyema INEC wakawashirikisha wadau wengine ili kufanya maboresho zaidi juu ya ugawaji wa majimbo hayo kwani vigezo vinavyotumika havitendi haki kwa maeneo mengine.

Olengurumwa amesema kuwa utaratibu wa sasa wa ugawaji majimbo haoni kama una uwiano sawa kwani kuna maeneo ambayo ni makubwa kijiografia lakini kuna majimbo machache na mengine ni madogo lakini yana majimbo mengi.

"Vigezo vinavyotumika kwa mijini, kwa majimbo inatakiwa kuwe na watu takribani laki 6 na mikoani kuwe na angalau watu laki nne. Sasa tujiulize kwa kuangalia vigezo hivyo vya watu na jiografia je utaratibu tulionao na idadi za watu kwenye wilaya unawiana na hivyo vigezo?

Kuna mikoa ina majimbo mengi lakini ukiangalia idadi ya watu ni ndogo sana na ukiangalia jiografia yake ni ndogo, na kuna mikoa ina majimbo machache ila ina watu wengi mfano mkoa wa Arusha una watu zaidi ya milioni 2.5 lakini kijiografia ni mkubwa sana na mjimbo ni machache sawa na Njombe na kwingine.

Lakini kuna maeneo kama Zanzibar ina eneo dogo lakini kuna majimbo 50."

Sambamba na hilo wakili Olengurumwa ameongeza kuwa, Wilaya ya Ngorongoro iliyopo Arusha ambayo kijiografia ni kubwa sana kwani Inakadiriwa kuwa na Mita za mraba 14,000 ambapo Mkoa wa Dar es salaam unaingia karibu mara 10 lakini ina jimbo moja ambalo lina muwakilishi mmoja, jambo linaloweka mazingira magumu kwa wakazi wa jimbo hilo kwenye hatua za kimaendeleo kwani hata mbunge wa eneo jimbo hilo akifanya ziara kwa kata zote, itachukua muda mrefu kulimaliza eneo lote hivyo kulazimika kutumia rasimali nyingi zinazoweza kupunguzwa endapo majimbo yataongezwa.

Kwa mujibu wa Majimbo yaliyopo, Mkoa wa Arusha wenye idadi ya watu takribani Milioni 2.5 una majimbo 7, ukiwa umezidiwa na maeneo yenye idadi ndogo ya watu kama vile Lindi yenye majimbo 9, Ruvuma (9),Songwe (6), Kaskazini Unguja (8), Mjini Magharibi (19), Kusini Pemba (9).

Back
Top Bottom