Olengurumwa: Huenda baadhi ya ripoti za tume na kamati zinazoudwa hushindwa kuwekwa wazi kwa sababu ya hofu

Olengurumwa: Huenda baadhi ya ripoti za tume na kamati zinazoudwa hushindwa kuwekwa wazi kwa sababu ya hofu

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za binadamu Nchini (THRDC), Wakili Onesmo Olengurumwa ametoa maoni kuwa uenda baadhi ya ripoti za Tume na Kamati mbalimbali ambazo huundwa kuchunguza masuala mbalimbali ushindwa kuwekwa wazi kwa kuwa taarifa zinaweza kuwa zinawagusa wenye mamlaka zinazohusika kuunda tume na Kamati hizo.

"Tumeshuhudia taarifa nyingi kutosomwa kabisa kutokana na kwamba kilichopo humo ndani pengine kinawagusa watu wengine ambao walitaka kuja kuzisoma hizo taarifa kwa Umma"Mratibu THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa

Amesema kuwa Kamati hizo zinaweza kuwa kuwa na hofu lakini amedai kuwa zina wajibu na kutoa taarifa za uchunguzi kwa umma huku akitolea mfano ripoti ya Mto Mara ambayo ilibua mjadala.

"Kimsingi Kamati hizo zinapaswa kutoa taarifa zao kwa umma, kama inapotokea changamoto fulani kama iliyotokea kwenye lile suala la Mto Mara tuliona hiyo Kamati iliundwa, vitu kama hivyo uwa wanaviogopa kuja kutoa taarifa kwa umma harafu taarifa hiyo ikaonesha pengine hamjaitoa kwa usahihi uwa wanaogopa 'criticism' ya umma." Mratibu THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa

Olengurumwa ameyasema hayo akitoa jumatano Novemba 16, 2022, wakati akizungumza kwa mlengo wa Haki za Binadamu na Utawala wa Sheria kupitia Twitter Space juu ya mada iliyoandaliwa na Mwananchi News Space kupitia Mtandao Twitter, isemayo "Matokeo ya ripoti zinazoundwa kuchunguza majanga na kupendekeza namna ya kuyakabili yanakidhi matarajio ya wananchi? Nini kifanyike?"
 
Back
Top Bottom