Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Akizungumza leo Julai 31, 2024 katika semina iliyowakutanisha watetezi wa Watoto kutoka Mikoa mbalimbali nchini, Mratibu Kitaifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC),Wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa kumekuwepo na wimbi la matukio ya ukatili kwa watoto ambalo linatakiwa kukemewa.
Amesema kuwa kutokana na ripoti ya Jeshi la Polisi ambayo iliyotolewa siku za hivi karibuni, inaonesha kushamiri kwa matukio ya utekaji wa watoto, ulawiti na ubakaji. Amedai kuwa ripoti hiyo inaonesha kuwa kwa mwaka 2023 pekee kulikuwepo na matukio takribani 73 ya utekaji wa watoto.
"Tunafahamu hali ya ulinzi wa Mtoto Nchi hii umekuwa na changamoto nyingi sana, Ripoti ya Jeshi la Polisi juzi ilionesha utekaji umekuwa mkubwa, kwa mfano mwaka jana (2023) tu watoto zaidi ya 73 kwa mujibu wa ripoti hiyo, tumeona masuala ya ulawiti na ubakaji yote yamekuwa matatizo makubwa ambayo hawa Watetezi wa haki za binadamu wanapaswa kwenda kukemea, kufuatilia na hata kuwajibisha zile taasisi ambazo zinahusika na ulinzi wa haki za Kiraia." amesema Olengurumwa
Licha ya hivyo amesema kuwa bado wataalamu wengi wa Serikali kwenye ngazi mbalimbali ambao wanasimamia ustawi wa watoto hawana uwezo wa kutosha pamoja na dhana za kukabiliana na changamoto hiyo, ameshauri Serikali kujenga utamaduni wa kuwajengea uwezo na kuwawezesha kuwa na zana za kukabili matukio hayo kwa wakati.
Ripoti ya Jeshi la Polisi ambayo imetolewa hivi karibuni inaonesha kwa mwaka 2023, matukio ya ubakaji yaliyoripotiwa ni 8,691 huku matukio ya ulawiti yaliyoripotiwa ni 2,448, ambapo inaonesha matukio ya ulawiti yaliyoripotiwa yameongezeka tokea mwaka 2021 ambapo Ripoti ilionesha kulikuwepo na matukio 1,114.
Itakumbukwa Julai 28, 2024 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni alipokuwa anazungumza kuhusu hali ya sintofahamu iliyoibuka kuhusiana na Watoto kutekwa na kupotea, alinukuliwa akisema Nchi ipo salama.
"Tunaenda vizuri kama Taifa, ajenda hazipo Mama anauburuza mwingi kweli, sasa haya ni maneno yanayotaka kututoa kwenye malengo tuache kujadili mafanikio ya awamu ya sita, Watu wazungumze vitu kama utekaji, utekaji uko wapi! Nchi ipo salama hii"alisema Waziri Masauni