Omari Mapuri, Ngwilizi, na Kavishe ndo pekee waliobaki wanaoufahamu Muungano - S.Sitta!

Mwikimbi

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2008
Posts
1,762
Reaction score
829
akizungumza juzi bungeni spika anayejiita kuwa ni spika wa viwango, aliwaambia wajumbe wa bunge kuwa ataawaalika watu watatu muhimu sana waliobaki wanaoufahamu muungano, baadaye imekuja kugundulika kuwa watu hawa si wengine bali ni makada wazoefu wa zamani wa ccm omari mapuri, kavishe na brigedia ngwilizi hawa wamewahi kuwa manaibu katibu wa ccm!

nataka kumuuliza sita kuwa ili uwe mweledi wa muungano ni lazima utoke ccm? ni lazima uwe katibu au naibu katibu wa ccm wa zamani ndo uwe na weledi tosha wa kuweza kuzungumzia muungano?

kuna watu kama proesa shivji amenadika sana kuhusu muungano na pengine kufanya tafiti nyingi lakini kwa viwango vya sita haujui muungano! Aboud jumbe Rais wa zamani wa zanzibar, jaji bomani, na wengine wengi kwa viwango vya sita hawaujui muungano.

ni vema mheshimiwa sita akafahamu kuwa huu si wakati tena wa bla bla, watanzania milioni 45 wanaufahamu sana muungano, hawahitaji ngonjera za akina mapuri, au kawishe au ngwilizi, bali wanataka watafiti wa kina kama akina shivji, jaji bomani, na wengine wasio egemea maslahi ya vyama kuwapa nuru zaidi na wala si hotuba ndefu
 
hivi kwa nini uamuzi wa wananchi usiheshimiwe? tayari wananchi wameshaamua wanataka muungano wa aina gani (yaani serkali 3 kwa kupitia tume ya warioba) hao wengine wanaoweza kutengua maamuzi ya wananchi ni akina nani hasa mpaka hata wawe na mamlaka hayo. hebu heshimuni uamuzi wetu tafadhali.
 
ningekuwa mimi ni mjumbe wa katiba nisingewasikiliza hao watu badala yake ningeenda mail mbili kula mbuzi.
 
Sishangai kwa nini unaitwa Abunuas, kwani kufikiri kwako kumekaa kama hekaya za abunuas. Hebu niambie ni wananchi wa wapi wameamua kuwa wanataka muunganao wa serikali tatu? watu 500,000 waliohojiwa na tume ya Warioba wanaweza kukilisha watu milioni 45? Inaonekana hata elimu ndogo ya kanuni za kutafuta sampuli ya uwakililishi hauna. Watu 500,000 ni wachache sana kuwakilisha watu milion 45, isitoshe kati ya hao mia tano ni asilimia 37 tu ndio waliotaka muungano wa serikali tatu. utasemaje kuwa hayo ni mawazo ya watanzania? Tafadhali usifanye mawazo yako kuwa mawazo ya watanzania wote.
 
MKUU kama ndo hivo mawazo yako ya upungufu wa takwimu hakuna hata haja ya kuijadili hiyo rasimu kwa kuwa nayo imetokana na sample size hiyo. TAFAKARI
 
inawezekana hatufanani katika kuchambua mambo. kati ya waTz mil 45 under 18 ni 14% ~to mil 6.5. sio kweli kuwa watu wote mil45 walikuwa na haki kisheria kutoa maoni. au we wenzetu hata huyo mtoto wako anayemnyonyesha alichangia au alikuwa na haki ya kuchangia? lakini pili hao waliotoa maoni ya serikali 3 ndo walikuwa wengi kuliko serikali 1 au 2. na hayo maamuzi lazima tuyaheshimu. overall hakuna aliyekatazwa kwenda kutoa maoni kwani tume ya warioba ilienda sehemu mbalimbali za nchi na walikuwa wakitangaza uwepo wao wa siku husika na sehemu husika. na la mwisho, kwani hofu yenu nyie ccm ni ipi? kama wananchi wanataka serikali 2 si hiyo rasimu italetwa kwetu kwa ajili ya kuipigia kura. sasa nyie hicho kimbelembele ni cha nini. fikirieni, chuweni hatua.

Sishangai kwa nini unaitwa Abunuas, kwani kufikiri kwako kumekaa kama hekaya za abunuas. Hebu niambie ni wananchi wa wapi wameamua kuwa wanataka muunganao wa serikali tatu? watu 500,000 waliohojiwa na tume ya Warioba wanaweza kukilisha watu milioni 45? Inaonekana hata elimu ndogo ya kanuni za kutafuta sampuli ya uwakililishi hauna. Watu 500,000 ni wachache sana kuwakilisha watu milion 45, isitoshe kati ya hao mia tano ni asilimia 37 tu ndio waliotaka muungano wa serikali tatu. utasemaje kuwa hayo ni mawazo ya watanzania? Tafadhali usifanye mawazo yako kuwa mawazo ya watanzania wote.
 
ningekuwa mimi ni mjumbe wa katiba nisingewasikiliza hao watu badala yake ningeenda mail mbili kula mbuzi.

Kama mimi ningekuwamo ktk bunge hilo basi ningemrushia hata kiatu huyo mpuuzi six kwani anaonyesha makucha yake ya u CCM, tafadhalini sana wabunge wetu mkikubali upuuzi wa aina hiyo basi mjue huku mtaani mnatuletea vita!
 
Sishangai kwa nini unaitwa Abunuas, kwani kufikiri kwako kumekaa kama hekaya za abunuas. Hebu niambie ni wananchi wa wapi wameamua kuwa wanataka muunganao wa serikali tatu? watu 500,000 waliohojiwa na tume ya Warioba wanaweza kukilisha watu milioni 45? Inaonekana hata elimu ndogo ya kanuni za kutafuta sampuli ya uwakililishi hauna. Watu 500,000 ni wachache sana kuwakilisha watu milion 45, isitoshe kati ya hao mia tano ni asilimia 37 tu ndio waliotaka muungano wa serikali tatu. utasemaje kuwa hayo ni mawazo ya watanzania? Tafadhali usifanye mawazo yako kuwa mawazo ya watanzania wote.

kama ndivyo,hofu ya watawala kutoitisha kura ya maoni kuhusu muundo wa muungano hapo kabla ya huu mchakato wa katiba mpya ilitoka wapi?
 
Hivi hata wanaopiga kura chaguzi nyingi hawazidi 40percent ya wapiga kura wote ...na ndio hao hao wanaomweka Rais madarakani sasa iweje 37 percent ya sampuli ya jaji Warioba muitolee mimacho
 
Back
Top Bottom