Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
OMARI MWARIKO NANI ANAMFAHAMU?
Huyo hapo chini aliyevaa kofia ni Omari Mwariko.
Nimemfahamu Omari Mwariko nakua na nasoma shule ya msingi Moshi katika miaka ya 1960.
Miaka hiyo Omari Mwariko alikuwa mtu maarufu sana.
Omari Mwariko ni msanii bingwa katika kuchonga na kazi zake zimeonyeshwa hapa nchini, Uingereza na Marekani.
Lakini kwa miaka mingi akawa kapotea katika ulimwengu wa usanii akawa haonekani wala hasikiki.
Siku moja miaka 13 iliyopita niko Moshi ghafla nikakutananae barabarani.
Nikamsalimia na nikajitambulisha kwa kumtajia jina la ndugu yake Athmani Upepo.
Hili jina "Upepo," si jina lake ila alipachikwa kwa ajili ya uwezo wake wa kukimbia mbio kwa kasi kubwa.
Nakumbuka utotoni Moshi kila mtu alikuwa na lakabu yake.
Kulikuwa na Ali Maresi.
Hili jina "Maresi," alipewa kwa uhodari wake mpirani kuwa akitanguliziwa pasi mpira akadodoshewa kwa mbele na kuupokea mabeki hawampati na atafunga goli.
Kulikuwa na Athumani Makufuta.
Kisa cha jina hili ni kuwa tukisomeshwa somo la Hand Craft Majengo Middle School na Mwalimu anaitwa Fritz (sina hakika na "spelling").
Huu ulikuwa mwaka wa 1963.
Mwalimu Fritz alichukia sana mwanafunzi kuchora kisha akafuta.
Adhabu yake ni viboko papo kwa papo.
Athumani akafuta na akala mboko sote darasani tunashuhudia.
Athumani Mfinanga toka siku ile akawa Athumani Makufuta.
In Shaa Allah iko siku nitaandika kuhusu haya majina na kuwatafuta wahusika ili tucheke.
Nitaanza na "Toligogo" Omari Matola golikipa hodari amefariki miaka michache iliyopita.
Sote tulikuwa wanafunzi wa Mwalimu Juma darsa yake baina ya Maghrib na Isha Msikiti wa Ijumaa.
Jina hili ukimwita lilikuwa na staili yake maalum.
Unalitamka kama vile unaimba.
Rafiki yangu Allah amrehemu kila nilipokutananae iwe Dar es Salaam au Moshi Mtaa wa Chini akiniadhimisha kwa mapenzi makubwa.
Turudi kwa Omari Mwariko.
Omari Mwariko alinipa muda wake na alipoona namdadisi sana kuhusu kazi zake pale pale akanikaribisha nyumbani kwake Njoro ili anioneshe baadhi ya vinyago alivyokuwa amechonga.
Nilifika nyumbani kwake na akanionyesha kazi zake na akachukua muda kunifungulia maktaba aliyohifadhi picha zake toka ujana wake alipoanza kuchonga.