Comred Mbwana Allyamtu
JF-Expert Member
- Jun 28, 2016
- 351
- 887
OMAR AL-MUKHTAR, SIMBA WA JANGWANI ANAYE TAZAMWA KAMA BABA WA TAIFA NA MWASISI WA TAIFA LA LIBYA, NI KIONGOZI ANAYE HESHIMIKA MNO ULIMWENGU WA KIARABU.
Na. Comred Mbwana Allyamtu.
Tuesday -20/11/2018.
“Hatuto jisalimisha, tutashinda (vita) au tutakufa....” (“we don’t surrender, We win or die”- Omar Al-Mukhtar 1931). Hayo ni maneno kutoka kwa Omar Al-Mukhtar kiongozi wa vuguvugu la ukombozi nchini Libya na Chad ambae hutazamwa kama baba wa mataifa hayo huku akipewa heshima kama babu na mwasisi wa ukombozi ukanda mzima wa mataifa ya kiarabu. Omar Al-Mukhtar ndie mwasisi wa vuguvugu wa kuzuia uvamizi wa wakoloni katika aridhi ya Afrika ambae alieendesha vita ya kupinga ukoloni (colonial resistance) kwa muda mrefu (miaka 20) kuliko kiongozi yoyote yule.
Omar Al-Mukhtar Muhammad Ibn Farhat Bredan alizaliwa Agosti 20, 1858 na kufariki dunia Septemba 16, 1931 kwa kunyongwa baada ya kuhukumiwa hukumu hiyo kwa kosa la kuendesha uasi dhidi ya utawala wa Italy ambayo ilikuwa ni koloni la Libya, Omar Al-Mukhtar anajulikana sana kama moja ya viongozi maarufu katika eneo la iliyokuwa koloni la Italia na alifahamika kama ‘’Matari wa Mnifa’’ yani “kiongozi aliye jitoa kwa ukombozi”, huyu Omar Al-Mukhtar alikuwa kiongozi aliyeongoza Upinzani dhidi ya uvamizi Libya hasa eneo la Mashariki mwa Libya eneo ambalo lilikuwa chini ya koo za Senussids, ambapo Omar Al-Mukhtar alisimama kupinga uvamizi wa Italy ndani ya Libya.
Omar Al-Mukhtar alikuwa moja ya viongozi muhimu na maarufu katika vuguvugu la Senussi ambalo ndio liloongoza harakati zote za kupinga uvamizi wa Italia ndani ya aridhi ya Libya, Al-Mukhtar anaonekana kuwa shujaa wa Taifa la Libya na ishara ya ukombozi wa taifa hilo huku akitazamwa kama mwasisi na baba wa taifa hilo akiwa ndio nembo ya ukombozi na upinzani dhidi ya dhulma za kiutu na kibinadamu katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislam.
Kuanzia mwaka wa 1911 Al-Mukhtar alipambana na kwa karibu miaka ishirini yote alilatibu na kuongoza harakati za upinzani dhidi ya Waitaliano ambao walikuwa ni wakoloni waliokuwa wameivamia Libya na kutaka kuitawala. Baada ya majaribio mengi ya kutaka kumtia nguvuni Al-Mukhtar kiongozi wa vuguvugu la ukombozi kushindwa, hatmae majeshi ya Italia yaliweza kumkamata Al-Mukhtar katika viwanja vya mapambano karibu na mji wa Slonta siku ya ijumatano saa tatu asubuhu na kisha baade kumuhukumu adhabu ya kunyongwa na hatmae alinyongwa mwaka 1931.
Omar Al-Mukhtar kiongozi anayekumbukwa mno huko Libya na eneo zima la Afrika ya kiarabu ambae ndie alie ongoza mapambano dhidi ya Ukoloni wa Kifaransa huko Chad na ule wa Uingereza kutaka kusalia kuikalia Misri pamoja na juhudi zake kubwa katika vita vya jangwani huko Senussid Mashariki mwa Libya na kuongeza hali ya ukombozi na mapambano dhidi ya ukoloni huko Afrika ya kaskazini anabaki kama baba wa ukombozi mioyoni mwa waarabu, huyu Omar Al-Mukhtar katika eneo zima la kaskazini mwa Afrika hutazamwa na kufananishwa kama Simon Bolivar kiongozi wa ukombozi wa bara la Amerika ya kusini ambae aliongoza ukombozi wa nchi za Venezuela,Colombia,Panama,Ecuador na Visiwa vya Costa Rika au Jose Martine Frosisca aliyeongoza ukombozi wa Agentina,Chile,Paraguay na Uruguay.
Haiba ya Omar Al-Mukhtar katika ukombozi wa Libya inabaki kuwa nembo ya taifa hilo huku kumbukumbu zake zilizo tukuka zikifutika katika historia ya Afika kwa kasi jambo linalo ondoa uhalali wa historia ya Afrika na damu za mamia zilizo poteza maisha katika ukombozi wa Walibya wakiongozwa na Omar Al-Mukhtar. Daima juhudi za Omar Al-Mukhtar ndani ya Afrika ya kiarabu ni Dinar yenye thamani isiyo futika daima, Kufatia hilo sasa turudi mpaka kwenye jangwa la Libya kwenye visima vya oasisi ya Kufra katika mji wa Kufrah kumtazama Simba wa jangwa na baba wa taifa la Libya Omar Al-Mukhtar Muhammad Ibn Farhat Bredan je ni mtu wa namna gani?
Omar Al-Mukhtar alizaliwa mwaka wa 1862 japo vyanzo vingine hudai alizaliwa mwaka 1858 kutoka kwenye familia masikini mno katika mji wa Zanzur karibu na jiji la Tobruk mashariki mwa Libya, Omari alizaliwa katika ukoo wa Mnifa, katika kanda ya Cyrenaica eneo ambalo lilikuwa chini ya udhibiti wa Ottoman (himaya ya Ottoman) kwa wakati huo. Wakati Omar alipokuwa kijana mdogo alipoteza baba yake mzazi hivyo alibaki na mama tu jambo lilomfanya kutumia ujana wake kutafuta unafuu wa maisha kwani alikuwa katika umaskini mkubwa sana, lakini baadae msamalia mwema aliyeitwa Sharif El Gariani mpwa wa Hussein Ghariani ambayo ilikuwa moja ya familia marufu nchini Libya aliamua kumchukua na kumsomesha na kumpatia huduma zote na baadae Omari alikuja kuwa kiongozi wa kisiasa na kidini huko Cyrenaica.
Omar Al-Mukhtar alipata elimu yake ya awali katika msikiti wa eneo hilo alilo zaliwa katika mji wa Zanzur, kabla ya kuendelea kujifunza kwa miaka nane katika Chuo Kikuu cha Senussi huko Jaghbub, mji mtakatifu wa Senussi Tariqa eneo ambalo lina waumini wengi wa kiislam ambao asili yao ni Uturuki. Al-Mukhtar alikuwa mtaalam na mjuzi katika elimu ya dini ya uislam na maarufu mno juu ya Koran na pia aliteuliwa kuwa imam na kiongozi wa waislam katika eneo zima la Jahgbub kuongoza waumini wa kiislam katika dhehebu la Sunn, alikuwa mstari wa mbele na alijenga mshikamano na ustawi wa vuguvugu la Senussi katika kuimarisha uislam eneo hilo. Kufatia hali hiyo Al-Mukhtar alikuja kufanywa kiongozi kwenye balaza la maamuzi la mji, kupitia ushilikiano wake na uaminifu wake na kuishi vizuri na watu katika jamii yake, hatmae watu wake walimchagua katika kamati ya haki ya mji wa Jaghbub katika kutatua migogoro ya kikabila.
Mukhtar alijenga uhusiano mzuri na vuguvugu la Senussid wakati wote wa miaka yake huko Jaghbub, mwaka wa 1895, Al-Mahdi Senoussi kiongozi wa vuguvugu la Senussi alisafiri pamoja naye kusini hadi eneo la Kufra, na wakati mwingine walikuwa nae katika safari nyingi zaidi hasa za kusini na pia Karo huko Chad, ambapo huku Al-Mukhtar alichaguliwa kuwa Sheikh wa Zawiyat Ayn Kalk (cheo cha kidini katika eneo maalum).
Wakati Ufaransa ikijiimalisha zaidi huko Chad mwaka wa 1899, Al-Mukhtar alipelekwa vikosi na watu wengine wa kutoka kwenye vuguvugu la Senussites ili kusaidia kulinda eneo la Chad kuto kuvamiwa kwa wavamizi wa Kifaransa, kwakuwa Senussi waliona kuwa upanuzi wa mataifa ya ulaya ni hatari kwa shughuli zao za Misionari katika eneo zima la Afrika ya Kati na Magharibi hivyo walitoa juhudi kuhakikisha uvamizi wa Ufaransa aushiki hatam eneo la Chad.
Mwaka wa 1902, Omar aliamua kurudi Libya baada ya kifo cha Al-Mahdi ambe ndio alikuwa kiongozi wa vuguvugu la Senissi, kiongozi mpya wa Senussi aliyeitwa Ahmed Sharif aliteuliwa kama kiongozi mpya wa Senussi alimteua tena Al-Mukhtar kuwa Sheikh wa Zawiyat Laqsur (cheo cha kidini katika eneo maalum) katika ukanda wa Cyrenaica ambapo ni eneo la Libya ya Kaskazini. Mnamo Oktoba 1911, wakati wa Vita vya Italia na Uturuki, Meri ya Italia iliyoitwa “Regia marina” ambayo ilikuwa ni meri ya Kiitaliano ya Royal Navy chini ya amri ya Admiral Luigi Faravelli ilifikia pwani ya Libya na kutia naga, katika eneo ambalo kwa kipindi hicho lilikuwa chini ya utawala wa Kituruki wa Ottoman.
Msimamizi huyo Luigi Faravelli alipofika hapo akamtahadharisha mtawala wa Kituruki kuwa wanatakiwa kusalimisha aridhi ya Libya kwa waitalia la sivyo wao watavamia na kuharibu haraka mji wa Tripoli na Benghazi. Waturuki na washirika wao wa Libya wakapata hofu na kuogopa kisha wakaamua waondoke kwenye nchi na kujisalimisha mbele ya italia, maana Waitaliano walitishia kuwa wangeipiga miji ya Tripoli na Benghazi kwa siku tatu. Hata hivyo eneo la mashariki mwa Libya waligoma kujisalimisha mbele ya Italia na hii ndio ilikuwa mwanzo wa vita kati ya majeshi ya kikoloni ya Italia na upinzani wa Mashariki ya Libya (Cyrenaica) chini ya kiongozi wao Omar Mukhtar vita ambavyo ilidumu kwa karibu miaka 22.
Huyu Mukhutar ambe alikuwa mwalimu wa Qur'an kwa taaluma, Mukhtar pia alikuwa na ujuzi katika maswala ya mapambano ya siraha na hasa mikakati na mbinu za mapigano ya jangwani. Alijua jiografia vizuri ya jangwa la Libya na alitumia ujuzi huo kwa faida katika vita dhidi ya Italia, maana maadui wake ambao walikuwa hawaijui vita vya jangwani hivyo ilimfanya kufanya vizuri zaidi kwenye mapambano wakati wote. Mukhtar mara kwa mara aliongoza vikundi vyake vidogo, vilivyo makini katika mashambulizi na kumfanya apate mafanikio dhidi ya Italia, baada ya mapambano ya usiku na mchana yeye na vikosi vyake walikuwa wanaweza kuhimili mapambano katika eneo la jangwa. Wanaume wa Mukhtar walishambulia kwa makini mashua, vikosi vya italia, na kukata na kuhabu miundombinu ya usambazaji na mawasiliano katika maeneo yote ya mapambano. Regio Esercito mkuu wa Jeshi la Kiitaliano katika vita hiyo alistaajabishwa uwezo wa vikosi hivyo vya Mukhtar huku akishikwa na aibu na mbinu zake za mapambano zishindwa kufanikiwa.
Baada ya italia kushindwa vibaya kwenye vita iliyopigwa katika eneo la mlima ya Jebel Akhdar "green mountan" mnamo 1924, Gavana wa Italia Ernesto Bombelli aliunda jeshi jingine lenye nguvu ya kupigana ili kuongeza nguvu ya kupambana na nguvu ya Mukhtar ambayo katika mapigano yote jeshi lao lilionekana kushindwa vibaya dhidi ya vikosi vya waasi ambapo jeshi hilo lilianza kuvunja ngome za Mukhtar mnamo Aprili 1925. Kufuatia hali hiyo Mukhtar alibadilisha haraka mbinu zake za mapambano na huku akiendelea kupokea msaada ulioendelea kutoka Misri. Mnamo mwezi Machi, mwaka wa 1927 licha ya majeshi ya Mukhtar kuuzibiti mji wa Giarabub tangu Februari 1926 lakini nguvu kubwa ya mapambano chini ya utawala chini ya Gavana Attilio Teruzzi, Mukhtar alishangaa askari wa Italia kuzidi kuongezeka huko katika mji wa Raheiba.
Kati ya mwaka wa 1927 na 1928, Mukhtar aliamua kuunda upya majeshi yake ya Senusiti, ambao walikuwa wakiwindwa mno na Italia. Pamoja na vita kuwa ndefu na ngumu sana hatimae Gavana Teruzzi alitambua sifa na uwezo za Omar Mukhtar za kuwa na uvumilivu wa kipekee na nguvu ya mapambano. Akaamua kusitisha vita na kuitisha mazungumzo ya amani. Gavana wa Libya tangu atangaze kusitisha mapigano mwezi Januari 1929, baada ya majadiliano makubwa yaliyofanyika na kuweka makubaliano na Mukhtar makubaliano ambayo yaliyoelezwa na Italia kuwa ni uwasilishaji wa makubaliano ya awali ya Italo-Senusite katika kutafuta amani ya kikanda. Italia ilichukua uamuzi huo baada ya kuona kuwa vita imekuwa ndefu sana yenye kuingizia Italia gharama kubwa katika kuiendesha.
Mwishoni mwa mwezi wa Oktoba 1929, Mukhtar alikataa maelewano na Italia baada ya kushindwa kuafikiana katika baadhi ya mambo maana Omar Mukhtar alisimamia msimamo wake kuwa lazima Libya iwe huru na waitaliano waondoke kweye aridhi ya Libya, kufatia hatua hiyo ya kupishana kwenye makubaliano Mukhtar aliamua kuendelea na mpago wake wa kuanzisha upya vita huku akiunganisha nguvu ya umoja wa vikosi vya Libya akiwaomba walibya kuungana katika kuuondoa utawala wa kiitaliano ambao ulikuwa umekalia aridhi yao huku vita hivyo akiipewa jina la “Libyan Mujāhidee”, akijitayarisha katika vita ambavyo yeye Mukhtar aliviita vita vya mwisho vya kuufurumisha utawala wa italia ndani ya Libya, Mkuu majeshi wa vikosi vya italia Rodolfo Graziani, ambae alikuwa kiongozi wa kijeshi wa Italia katika vita nchini Libya kutoka Machi 1930 akaamua na yeye kutangaza vita rasmi na Mukhtar.
Katika mapambano ya mwezi wa Juni vikosi vya Mukhtar vilishindwa vibaya, Graziani alianzisha mpango mpya wa mapigano wa kuvunja na kusambaratisha vikosi vyote vya ukombozi vya Mukhtar ambavyo vilikuwa vikingoja mapigano ya Mujāhidee ndani ya Libya. Katika mpango huo italia iliwahamisha wakaazi karibu Idadi ya watu 100,000 kutoka kwenye eneo la Jebel Akhdar kupelekwa kwenye makambi kupisha mapigano makali ya kutokomeza waasi waliokuwa chini ya Mukhtar, huku upande mwingine mpaka wa Libya na Misri kutoka pwani ya Giarabub ikafungwa kuzuia msaada wowote wa kigeni kuingia kwa wapiganaji pamoja na kuwanyima msaada kutoka kwa wakazi wa eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuchoma moto mazao na vyakula vyote ili kuwafanya wapiganaji wa Mukhtar wasipate chakula wakati wote wa vita.
Hatua hizi, ambazo Graziani aliziazisha mwanzoni mwa 1931, zilipata mafanikio dhidi ya Senusite. Kwani Waasi walipunguziwa msaada na vifurisho vingi vilivyo wapa nguvu katika kuendesha vita, kwani hata vyakula vidogo vilivyo patikana na kusafirishwa kwa waasi vilipigwa na ndege ya Italia, huku vikosi vya italia walifuatilia kwa ukaribu vikwazo vyote kuhakikisha askali wa Mukhtar awapati chakula wa silaha kutoka mahali popote. Mpango huo ulisimamiwa chini ya vikosi vya Italia vikisaidiwa na waandishi wa habari na washirika waitalia.
Mukhtar aliendelea kupigana licha ya matatizo kuoongezeka na hatari ya yeye kushindwa vita ilianza kuonekana, katika mapambano ya mwezi Septemba 11, 1931, vikosi vya Mukhtar vilizidiwa nguvu na kusogezwa mpaka karibu na mji wa Slonta. Kutoka kwenye mji huo Mapambano ya Mukhtar ya karibu miaka ishirini ikahitimishwa mnamo tarehe 11 Septemba 1931, baada ya Omar Mukhtar alipojeruhiwa na baada ya vikosi vyake vya mwisho kupigwa vibaya na askali wengi kuuwawa katika vita hiyo ya Slonta, kisha Muktar alitekwa na kukamatwa na jeshi la Italia na vita hiyo ya jangwani ikaishia hapo.
Waislamu wengi duniani walimpa heshima na tuzo kutokana na Ustahimilivu wake ambao umekuja kuathiri ukanda wa Afrika kaskazini kipindi cha kudai uhuru hasahasa wafungwa wake waliotumikia jela ndio walio kuja kuanzisha vugu vugu la uhuru wa Libya mwaka 1956, Mukhtar ambaye alisisitiza juu ya ushikamanifu wa kitaifa na kupinga dhuruma ya kikoloni. Mukhtar alizungumza hayo mara kwa mara kila alipo soma mistari ya amani kutoka kwenye Qur'an tukufu.
Baada ya kukamatwa na vikosi vya kiitalia siku ya tatu, Mukhtar alishtakiwa kwa kosa la kuendesha uasi dhidi ya utawala wa Italia na kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa mpaka kufa, hatimae tarehe 14 Septemba 1931, mahakama ya kikoloni iliyokuwa chini ya utawala wa Italia ilitoa hukumu ya Mukhtar kutumikia adhabu ya kunyongwa hadharani mpaka kufa. Kabla ya kunyongwa Omar Mukhtar aliulizwa kama angependa kusema maneno ya mwisho mbele ya mahakama, lakini Mukhtar alijibu kwa maneno ya Quran kwa kusema "Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwa kweli sisi tunarudi kwake".
Mnamo Septemba 16, 1931, kwa amri ya mahakama ya Italia Omar Mukhtar alinyongwa mbele ya umma na wafuasi wake katika kambi ya POW iliyopo katika mji wa Suluq akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kunyongwa mwili wake ulichukuliwa na maafisa wa Italia na kuzikwa. Baada ya kifo cha Omar Mukhtar vita nchini Libya vikamalizika na utawala wa Italia ukashika mizizi japo wafuasi wa Omar Mukhtar waliendele na vuguvugu la kudai uhuru bila kukoma na hali ilienedele mpaka mwaka 1951 baada ya italia ilipoamua kukabidhi uhuru wa bendera kwa mfarme Idrisa l ambae nae alikuja kupinduliwa na Muamar Ghadaf mwaka 1969.
Pamoja na mchago wake mkubwa Omar Mukhatr katika harakati za ukombozi Libya na duniani kote siku ya kifo chake ni siku ya kitaifa nchini Libya na baadhi ya chi za kiislam kama Syria,Tunisia Chad na Misri katika kipindi cha utawala wa Abdul Gamal huku picha yake Mukhtar imewekwa kwenye sarafu ya dinari ya Libya. Nje na hayo pia sanamu lake kubwa limetengenezwa huko Caracas Venezuela kama kumbukumbu ya kuenzi mchango wake katika harakati za ukombozi wa mwanadamu duniani.
Miaka ya karibuni filamu maarufu ilionyeshwa na kusimulia namna vita ya kupinga uvamizi nchini Libya ilivyoendeshwa, filamu hiyo ilipewa jila la “The lion of Desert” (Simba wa Jangwa) filamu hiyo ilichezwa mwaka 1981, na aliye cheza nafasi ya Mukhtar alikuwa nyota maarufu aliyeitwa Anthony Quinn, akishilikiana na wengine kama Oliver Reed, na Irene Papas. Ambayo ilionesha historia nzima ya mapambano ya Mukhtar dhidi ya vikosi vya Rodolfo Graziani. Mataifa mengi ya kiarabu mwanzoni yalituhumu filamu hiyo na ilipingwa na Waarabu na Waislamu kwa kudai kuwa inakashifu ushujaa wa Omar Mukhtar na kudaiwa kuficha mambo kadhaa mpaka hapo ilipokuja kufanyiwa uhariri mwaka 1986 ambapo ndio ikaja kuungwa mkono.
Omar Al-Mukhtar Muhammad Ibn Farhat Bredan ni kiongozi anayepewa heshima sana ndani ya Libya kwani mwaka 1961 Chuo Kikuu cha Omar Al-Mukhtar kilianzishwa na kupewa jina lake kwa heshima yake , lakini pia mwaka wa 2009, kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alikuwa amevaa picha ya Mukhtar kwenye aina ya mavazi yake kwenye kifua chake wakati wa ziara ya Roma nchini Italia, huku Gaddafi mwenyewe akiita ziara ile kuwa ni “kumlejesha mwana wa zamani wa Mukhtar katika aridhi ya Italia”.
Pamoja na Vita vya wenyewe kwa wenyewe ndani ya Libya vilivyo anza Februari 17, 2011, Omar Mukhtar ndio alikuwa alama ya Libya huku wakidai umoja na huru dhidi ya utawala wa Ghaddafi na picha yake ilionyeshwa kwenye bendera na bango la Libya wakati wa mapambano. Huku Majeshi ya kiasi yaliita moja ya brigade yao jina "Omar Mukhtar brigade" wakionesha kuwa wao ni wafuasi wa Mukhtar. Pamoja na hivyo huko Marekani msikiti wa huko mji wa Tampa, Florida, USA, ulipewa jina la Masjid Omar Al Mokhtar kwa kuonesha heshima ya kiongozi huyo. Mitaa kadhaa duniani imepewa jina lake kwa heshima yake huku moja ya mitaa hiyo ni ule wa Jiji la Gaza, inayoitwa Omar Mukhtar Street. Mwingine ni ule wa Cairo, Misri, inayoitwa Omar Al Mukhtar Street.
Pia kule Qatar Mitaa kadhaa imepewa jina lake kwa heshima ikiwa ni pamoja na katika eneo la West Bay la Doha, Qatar inayojulikana kama "Omar Al Mukhtar Bay". Huku nchini Tunisia, mji wa Bizerta umepewa jina la Mukhtar city. Ikiwa ni pamoja na Barabara kuu ya mji mkuu wa Riyadh, Saudi Arabia umepewa jina la Omar Al Mukhtar Road. Pia katika mji wa Irbed nchini Jordan mitaa kadhaa imeitwa jina lake.
Huyu ndio Omar Mukhtar Simba wa Jangwani aliepigania nchi yake ya Libya kutokana na dhurma iliokuwa ikitendwa na wakoloni wa kitaliano dhidi ya raia wa Libya, Umar Mukhtar (Omar Mukhtar) akiwa Imam na kiongozi wa kidini katika eneo lake hakuwa tayari kuruhusu udhariri juu ya jamii yake..
Huyo ndio Omar Mukhtar Mwafrika asietajwa sana katika history ya Afrika..
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com