Ombamba maarufu, Matonya, afariki dunia




Ingawa marehemu mzee Matonya aliingia kwenye vitabu vya historia ya Tanzania kwa kile waingereza waitacho wrong reason, ameacha somo kubwa kwa wenye kufikiri. Taarifa zilizotufikia ni kwamba mzee huyu maarafu kama alama ya umaskini na ufisi wa taifa letu amefariki dunia. Mzee huyu mwenyeji wa Dodoma alikuwa kivutio kwa wengi jijini Dar Es Salaam ambapo yalikuwa makao makuu ya shuguli zake za kuomba. Kipindi fulani alimtoa jasho mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam wa wakati ule Yusuf Makamba alipomuamuru ahame na kuachana na shughuli za kuomba kwa sababu alikuwa akilidhalilisha taifa. Matonya hakukubali kufa kibudu. Alipambana na Makamba hadi kumtishia kuwa angemng'oa kwenye nafasi yake.

Sababu kubwa aliyotoa Matonya ni kwamba akina Makamba walikuwa walafi wanaokula kwa mikono na miguu huku wengi wakiangamia. Hivyo, kuomba kwa Matonya ilikuwa ni haki yake. Na kweli, kuomba ni bora kuliko kuiba au kujihusisha na ufisadi, mihadarati na jinai nyingine ambazo zimelifikisha taifa letu lilipo. Kwetu sisi Matonya alikuwa matunda ya siasa za kifisi na ubabaishaji. Pia Matonya alikuwa alama na kumbukumbu kwa wenye akili kuwa mambo hayakuwa sawa. Ni bahati mbaya kuwa watawala wetu hawakujifunza suto lililotokana na shughuli za Matonya. Badala yake walitaka kutumia maguvu kumficha ili asiwaudhi wao na wageni wao hasa wafadhili. Hakika huu mchezo umekuwa ukiendelea hata nje ya nchi ambapo wazungu huja Tanzania na kupiga picha za watu maskini na kuzipeleka kwao kutegeneza mabiloni kwa kisingizio cha kuhamasisha watu wao matajiri kuwachangia waswahili wenye dhiki. World Vision linaongoza kwa jinai hii. Inashangaza ni kwanini mamlaka zetu haziwazuii hawa wafanya biashara ya nafsi za watu kupiga hizo picha.

Tukirejea kwa Matonya, alikuwa shujaa aliyewabana watawala wetu. Hata walipowaficha maskini wengi vijijini, yeye alikharifu hujuma hii na kujitokeza na kuomba hasa jijini Dar Es Salaam ambapo ni moyo wa nchi. Matonya atakumbukwa Dar Es Salaam, Dodoma na Morogoro (alikoweka makao yake ya muda baada ya kutimuliwa kwa muda mfupi na Makamba kabla hajamdharau na kumshinda na kurejea Dar.)

Kifo cha Matonya ni pigo kwa taifa hasa maskini aliowawakilisha kwenye uso wa nchi kwa kung'ang'ania kuomba badala ya kuiba. Inashangaza watawala wanaosifika kwa kuombaomba kumfukuza ombaomba mwenzao. Je ni kwa sababu hakuwa ombaomba mwenye suti au anayetumia kalamu?
Nenda kapumzike mzee Matonya ulikuwa changamoto kwa wenye akili na udhu.
 
Duh,somo zuri na pana mno,kumbe ndio maana hata JK always anaitwa matonya,ok R.I.P Babu.
 
RIP Matonya. Angalau profession yako ina wateja wengi siku hizi. Pumzika kwa amani.
 
kila nafsi itaonja mauti....RIP kamanda Matonya.........

RIP fellow ccm victim MATONYA

Sahihisho kidogo: Siyo kweli kwamba kila nafsi itaonja mauti!!! Enock na Elijah walichukuliwa kwenda mbinguni wakiwa hai hawakuonja mauti na siku Yesu mwana wa Mungu aliye hai atakaporudi wafuasi wake watakao kuwa hai siku hiyo hawatakufa bali watanyakuliwa mawinguni bila kuonja mauti. Believe in him who gives life, he came so that they may have life and have it more abundantly
 
Nakumbuka maneno yake kuwa kwenye riziki hapakosekani fitina. Poleni wafiwa.
 
Alikula chumvi nyingi sana mzee matonya!!! "Matonya na makamba,city na wamachinga"-Prof Jay
 
R.I.P Matonya, uliwakilisha wanyonge na maskini. Wako wengine wengi wa aina yako umewaacha ila noa siku moja wataonja mauti, ni kila mmoja wetu hata awe billionaire!!! Wameweza hadi robot but wameshindwa kupulizia roho!!
 
R.I.P Matonya,Sasa hapo dilemma kwa mkuu w kaya,je aende kwa zenawi au matonya!!?

I SWEAR ATAENDA KWA DICTATOR ETHIOPIA! By the way atatuma salamu za rambirambi na ubani (some shillings) kwa LATE MATONYA then basi...
 
mmoja ni ombaomba wa ndani na mwingine ni ombaomba wa ulaya na ni marufu sana ulaya kwa kuombaomba kama alivyo MATONYA alinyo marufu hapa TZ..

UKWELI UNAUMA LAKINI USEMWE TU... M.K.W.E.R.E. ni matonya. ah sore jk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…