Hivi hii thread ina maana wajasiriamali wote (wafugaji) hawajaiona ama!!Maana ni muda mrefu sasa na nadhan mleta ombi hajafanikiwa kwenda kumtembelea mfugaji hata mmoja.
Inawezekana ikawa haya yafuatayo:
1. Hakuna wafugaji halisia hapa Jf zaidi ya kujisifia na maelezo ya kijasiliamali,kupost picha za mifugo na kuleta porojo nyingi za kiujasiliamali.
2. Kutojiamini kwa wafugaji, kama wapo lkn,pindi watakapotembelewa na kukuta utofauti wa uhalisia wa ufugaji na maelezo waliyoyatoa humu Jf.Watu hutoa picha za kuku,bata,mazao n.k inawezekana wana download na kuzipost hakuna kitu wanachokifanya.
3.Ubinafsi,kutotaka mwenzako nae afaidike kutokana na kufaham kiuhalisia njia za ufugaji wako
4.Imani potofu,huenda watu wakahisi kwamba utakapomtembelea na kuona mifugo yake mambo yanaweza kwenda mrama kama Wizi n.k
Kama yote hapo juu ni HAPANA kwanin sasa hakuna aliyejitokeza zaidi ya kumshaur asubir Maonyesho ya 88? muda wote wa kusubiri 88 wa nin wakat wafugaji wapo kibao hapa?Wengine wanauza kuku 100,wengine wana uwezo wa kusupply bata 50 hao wote wako wapi?
Hebu Tukubali ombi lake wajamen la huyu mwanachama tuache longolongo!!!