Ombi kwa Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Mawasiliano: Tunaomba mtupie jicho kwenye kupanda kwa ma-bando (Mobile internet services)

Ombi kwa Rais wetu Mhe. Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Mawasiliano: Tunaomba mtupie jicho kwenye kupanda kwa ma-bando (Mobile internet services)

codes

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2015
Posts
344
Reaction score
514
Videkezo.

[1]Mpaka TTCL wamepandisha bei za mabundle kutoka 1.2GB /1000 Tshs mpaka 600MB/ 1000 Tshs. Makampuni binafsi yalipandisha kitambo.

[2]Inavyooneka, makampuni ya simu yanashirikiana kupandisha bei za ma-bundle kama madereva wa dala dala stand ya 7 7[Dodoma]. Wakishapandisha wote, unaenda wapi

Kutokana na mabadiliko ya science na technologia, SOCIAL MEDIA ndo chanzo kikubwa cha taarifa toka pande zote za dunia [Socia Media zinabeba TV,Radi0,magazeti]. Social media inahitaji internet [Ma-bundle], Internet ndo maisha kwa sasa. Kwenye internet tuna-material ya kujisomea vyuoni mashuleni, makazini[kuongeza ufanisi], tunapata hardwares zenye computational kubwa kama colabaratory.

Raisi mpendwa ulishawahi kuliongelea hili swala ya mbundle [Mobile internet services] kwamba ZISHUKE, [wakati Daktari wa binadamu alipoiongoza wizara ya mambo ya IT/ICT] lkn walishusha kwa muda kidogo , wengine hawakushusha kabisa, baada ya muda wakapandisha karudi pale pale. TTCL ndo wamekuwa wa mwisho[leo tare 19/10/2021] kurudi kwenye gharama ulizotaka zishuke[Hii inamaanisha makampuni ya simu yameikaidi].

Tunaomba mama yetu mpendwa uliangalie hili la kupanda kwa ma-bundle kwa mara nyingine ili usiwape watu faida ya maneno na kutusaidia watumiaji wa hali ya chini. Pongezi wa Serikali ku-implement mkongo wa taifa...., ulishusha gharama za internet .....ila sasa tunakoelekea internet inaenda kuwa anasa.
Ahsante.

Mwananchi.
I
 
Videkezo.
[1]Mpaka TTCL wamepandisha bei za mabundle kutoka 1.2GB /1000 Tshs mpaka 600MB/ 1000 Tshs. Makampuni binafsi yalipandisha kitambo.
[2]Inavyooneka, makampuni ya simu yanashirikiana kupandisha bei za ma-bundle kama madereva wa dala dala stand ya 7 7[Dodoma]. Wakishapandisha wote, unaenda wapi

I
Nisikilize kwa makini, hivi unadhani serikali inafurahia Sana wananchi walivyo na access ya taarifa mbalimbali za ndani na nje ya nchi?

Kwa kuwa haifurahii, Basi wanafurahia Sana bando likipanda maana mapato yake yanaongezeka (serikali) na namba ya watu wanaopata access kwenye taarifa/ information inapungua.

Serikali nyingi za Afrika zinaiogopa mitandao ya kijamii haswa kwa like kilichotokea hapo Afrika ya Kaskazini na mashariki ya Kati miaka michache nyuma.

Serikali zinapenda majority muwe bongolala ili ziweze ku run smoothly, Mambo ya kuhojihojiwa haipendi kuyasikia, Mambo ya kukosoakosoa, Mambo ya mawazo mbadala, hasa Yale mazuri zaidi . Wanataka kila wazo zuri litokee kwao
 
Wafute bando zote tu, tuwe kama zamani mb 1 inakatwa sh 2000 kwenye muda wa maongezi .
IMG_20210811_103656.jpg
 
Zingatia hili.
kila kitu kimepanda. Na serikali iko kimya. Walipozuia bei ya fuel kwa mwezi mmoja walikuja na nyaraka za kupongezana ila mwezi wa 10 si yalipanda? Tusubr Nov yatapanda tena na bidha zake zote
almnimium dirisha 4*5 ilikuwa 200 ila sasa ni 300-340 tena material Ni adim....mambo ni balaa tupu
 
Imebaki wafanyabiashara wanajipandishia bei hovyo kwa sababu hakuna bei elekezi ya serikali
 
Kwakeli Hali ni mbaya mno kila kitu bei juu sijui tunaelekea wapi kila uchwao maisha yanapanda, ajira hakuna, wanetu, baba, mama ambao not wamachinga kila leo wanatolewa mijini wanajitafutia ridhiki watoto wasome, wale na kivaa mambo yanawawia vigumu.

Akumbukwa JPM na ataendelea kukumbukwa maana imeshakuwa kero, watu wanapeana madaraka makubwa kila uchwao kwakweli inahuzunisha na kustaajabisha...
 
Back
Top Bottom