Ombi kwa Serikali: Madalali wote Dar es Salaam watambuliwe na wasajiliwe

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Posts
20,561
Reaction score
24,428
Kutokana na tatizo la ajira kuwa kubwa tunashuhudia vijana wengi kujiingiza katika shughuli mbalimbali wengi wapo kwenye bodaboda na kundi kubwa pia limejiingiza kwenye udalali wa aina mbalimbali.

Kwa jinsi bodaboda wanavyotambuliwa kwa vyombo vyao tunaiomba serekali yetu iwatambue madalali wote hapa nchini hasa zoezi lianze kwa madalali wote wa mkoa wa dar es salaam, watambuliwe, kwa nida, wawe wamesajiliwa, wamelipia vitambulisho vyao ambavyo vitakuwa na namba maalumu ya utambulisho wake ambayo itakuwa searchable katika menyu za simu zetu.

Hili litakapofanyika litasaidia sana vitendo viovu kuondoka pia litasaidia usalama wa taifa letu kwani dalali atachunguza kwa makini mpangaji wake anayempeleka mahala ili matatizo yasijemrudia yeye kwa kupeleka mwovu mahala fulani, pia wateja wao watakuwa na amani.
N. B, watanzania wengi mno wanapigwa fedha zao na wanakosa pa kwenda, hasa madalali wa Viwanja N. K.
Watakapotambuliwa rasmi na kuwa na vibali maalumu hata nao watasaidika juu ya haki zao 5%.
 
Madalali Dar naona wanaendekezwa Sana,
Eti mtu Hata nyumba ya kupanga Mpaka Dalali?. Na unakuta Mpaka mmiliki anaogopa kukupabgisha bila Dalali, ni ujinga.
 
Kwa jinsi madalali walivyo wengi kuliko wateja, serekali inapoteza fedha nyingi mno kwani kila dalali ili atambulike na akidhi alipaswa kupewa leseni ya udalali,
Sisi wateja wahitaji wa vyumba tungewekewa katozo la kutotumia dalali ambaye hajasajiliwa na ni fursa hata kwa halmashauri kuona na kuanzisha hili,wangejiongezea kipato.
 
Kutokana na tatizo la ajira kuwa kubwa tunashuhudia vijana wengi kujiingiza katika shughuli mbalimbali wengi wapo kwenye bodaboda na kundi kubwa pia limejiingiza kwenye udalali wa aina mbalimbali.

Kwa jinsi bodaboda wanavyotambuliwa kwa vyombo vyao tunaiomba serekali yetu iwatambue madalali wote hapa nchini hasa zoezi lianze kwa madalali wote wa mkoa wa dar es salaam, watambuliwe, kwa nida, wawe wamesajiliwa, wamelipia vitambulisho vyao ambavyo vitakuwa na namba maalumu ya utambulisho wake ambayo itakuwa searchable katika menyu za simu zetu.

Hili litakapofanyika litasaidia sana vitendo viovu kuondoka pia litasaidia usalama wa taifa letu kwani dalali atachunguza kwa makini mpangaji wake anayempeleka mahala ili matatizo yasijemrudia yeye kwa kupeleka mwovu mahala fulani, pia wateja wao watakuwa na amani.
N. B, watanzania wengi mno wanapigwa fedha zao na wanakosa pa kwenda, hasa madalali wa Viwanja N. K.
Watakapotambuliwa rasmi na kuwa na vibali maalumu hata nao watasaidika juu ya haki zao 5%.
Tena kuna leseni yao toka enzi za mkoloni, hiyo kazi inaitwa "commission agent".
 
Labda kwa nyakati hizi, leseni zao zingewekwa katika category 3, ndogo, ya kati, hiyo kubwa, nalia na hawa jamaa kwa nguvu zote kwa sababu ndio chanzo cha hata migogoro mingi ya Viwanja na mambo mbalimbali.
 
Back
Top Bottom