Emanueli misalaba
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 1,769
- 2,523
Ombi kwa serikali iwasaidie wananchi wa Fuoni meli tano sheli, shehia ya Mnarani, kuhusu nyumba namba SH. MNR. 08/101
Ni kero zaidi ya kero kwenye mtaa, wanauza pombe za bia wakiwa hawana leseni pia pombe za kienyeji aina ya gongo na bangi wakati pombe hizi ni haramu kwa mjibu wa sheria,
Wanashirikiana na nyumba ya pili namba SH. MNR. 08/107,
Wananchi wamelalamika sana ofini kwa sheha bila mafanikio, kwani kiongozi wa mtaa Bwana Sheha
amejitahidi sana ameshindwa kwa sababu muuza gongo ana mtu wake usalama wa taifa anampa jeuri na kiburi.
Muuzaji mkuu amewahi kukamatwa na mkuu wa mkoa wa kipindi hicho akiwa Mjini Magharimbi Rc Ayoub Mohammed na kuifunga nyumba yake kwa kufuli, muuzaji gongo huyu aliwekwa ndani kwa miezi kadhaa ndani, baada ya Mh Ayoub Mohammed kuhamishwa mkoa, muuzaji huyu wa gongo alitolewa na kurudi kuendelea na biashara ya gongo huku akifanya sherehe na kuweka magoma kuwaonyesha majirani na watu wa mtaani yeye ni mbabe hawamuwezi.
Huku ikidaiwa ana ndugu yake ni usalama wa taifa mkubwa anampa kiburi cha kuendelea kuharibu vijana na nguvu kazi ya taifa.
Mama huyu anakusanya walevi wa Sehemu nyingi hapo utakuta wa kutoka mitaa Kinuni, Kwerekwe, Tomondo, Chunga nk nk, na anaharibu hata baadhi ya vijana wa mtaani nyumba yake haina ukuta, wateja wake hukaa pembezoni mwa nyumba za majirani inakuwa kero hasa wakilewa,
Nyumba nyingi zilizo karibu na huyu muuza gongo hazina taa za nje kwani wateja wake huvunja taa, kuchanwa nyavu za kwenye madirisha ukijisau wanapita na simu, wakilewa kelele, fujo, matusi mazito mazito hupigana saa nyingine hadi huumizana,
Ni ombi langu kwa serikali kuu ichukue hatua juu ya hawa wauzaji ili kuokoa vijana na jamii.
Hata kama huyo ndugu yake amemweka ki mission hapo mtaani ndo awe anauza vitu haramu gongo, bangi na madawa ya kulevya?
Je, kwa mjibu wa sheria za nchi inaruhusiwa?
Kama yuko kwenye mission, mission gani yao isiyoisha miaka karibu 10?