Ombi kwa wanachama na wakereketwa wa upande wa pili

Ombi kwa wanachama na wakereketwa wa upande wa pili

Joined
Jan 16, 2019
Posts
19
Reaction score
62
Nitangulize shukrani zangu za dhati kwa wale wote watakao pitia/pita katika uzi huu. Nawashukuru nyote/wote.

Ni matumaini yangu kuwa nyote/wote mko "buheri" wa afya na naendelea vyema "kupambana" kupata mkate wa siku, kwa walio wengi, nakupata mpake wa siku na ziada kwa wale wachache.

Mimi niko pia niko "buheri" wa afya, na zaidi, naendelea kupambana kupata mkate wa siku kama walivyo/ilivyo kwa walio wengi.

Kama kichwa cha uzi/bandinko hili linavyojielezea, ningependa kuwaomba sana ndugu zangu/zetu hasa wale wa upande wa pili, ikiwapendeza wawe wanatuletea taarifa ya moja kwa moja toka mahakamni, "live updates" kulingana na shauri linalomkabiri aliyekua mkuu wa wilaya, wa wilaya moja kati ya zile wilaya zinazopatikana mkoa wa Kilimanjaro.

Lengo/kiini cha ombi/maombi haya ni kuweza kusaidia/kuwezesha walio wengi humu jamvini kufahamu kila kinachoendelea katika shauri hilo, kama vile hawa wa upande huu wanvojitahidi kuleta jamvini kila kinachoendelea katika shauri liloko mahakamani likimuhisisha Mwenyekiti na wale waliokua "waajiriwa" makomandoo katika jeshi letu la Wananchi Tanzania.

Ninaamini kwa hawa wa "upande" wa pili kuleta taarifa za moja kwa moja toka chumba cha mahaka, sio tu kitatoa fursa kwa umma kupata taarifa sahihi kwa wakati, bali itakua ni fursa kwa walio wengi kufamu/kupata moja mbili "ABC" ama "shule"inayohusu/zinazohusu namna mahakama inavotafasiri/tafsiri sheria ili kutenda haki hasa katika mashuri yanayohusu jinai.

Ninawasilisha. Niwatakie nyote/Wote wakati mwema.
 
Marafiki wakati wa raha na ukiwa nacho utawapata wengi sana.
Wakati wa shida hutawaona.
Mmoja aliandika kumpongeza Rais kwa demokrasia za mahakama.
Ila hakusikika kuandika baada ya hukumu ya DC
 
Back
Top Bottom