Mfichua maovutz
Member
- Oct 3, 2022
- 5
- 3
Kwa:
Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora,
S.L.P 2483,
Dodoma.
YAH: OMBI LA KIBALI KWA WAHITIMU WA KOZI YA DIPLOMA IN PIPE WORKS OIL AND GAS ENGINEERING KUOMBA NAFASI ZA AJIRA ZA UFUNDI BOMBA
Ndugu Katibu Mkuu,
Kwa heshima na taadhima, mimi ni mwakilishi wa wahitimu wa kozi ya Diploma in Pipe Works Oil and Gas Engineering, ambao tumehitimu mafunzo yetu katika vyuo vya Arusha Technical College na NIT. Kupitia tangazo rasmi la ajira za serikali lililotolewa hivi karibuni, tumebaini kwamba zipo nafasi za ajira za Fundi Bomba ambazo zinaendana moja kwa moja na ujuzi na mafunzo tuliyopata.
Hata hivyo, kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa kwenye tangazo hilo la tarehe 13 desemba 2024 kuna hitaji la kupata kibali kutoka kwa Ofisi yako tukufu ili tuweze kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kuomba nafasi hizo za ajira. Tunatambua umuhimu wa kufuata taratibu zote za ajira za serikali na tuko tayari kushirikiana kikamilifu ili kuhakikisha tunapata nafasi ya kutumia ujuzi wetu kuchangia maendeleo ya taifa.
Kwa msingi huo, tunakuomba kwa heshima ukubali ombi letu na kutoa kibali kinachohitajika ili sisi wahitimu wa kozi hii tuweze kushiriki katika mchakato wa kuomba nafasi za Fundi Bomba kama ilivyotangazwa. Tuna imani kuwa ujuzi wetu katika Pipe Works Oil and Gas Engineering utachangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha miradi mbalimbali inayohusiana na sekta ya maji,mafuta na gesi nchini.
Taarifa zote za Kozi hii zinapatikana Chuo cha Ufundi Arusha.