Ombi la kuimarisha usalama na kulinda amani ya wananchi dhidi ya vitendo vya utekaji Tanzania

Bwana kaduga

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2018
Posts
863
Reaction score
1,812
Nawasalimu kwa jina la JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.

MH. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR. SAMIA SULUHU HASSAN,

Kwa heshima na taadhima, napenda kukuandikia ujumbe huu nikiwa na imani na uongozi wako thabiti unaoongoza taifa letu la Tanzania. Tumekuwa tukisikia kwa muda sasa kuhusu suala la utekaji na mateso yanayowakumba baadhi ya wananchi, hususan watoto wadogo. Hali hii imeleta hofu mitaani na vijijini kote nchini, na imeleta changamoto kubwa kwa familia nyingi.

Rais, nikiwa kama mmoja wa raia wako, nakuomba kwa unyenyekevu kuwaongoza vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu katika kulinda amani ya wananchi na kuchukua hatua stahiki dhidi ya wahalifu wanaotishia usalama wa taifa letu. Sisi wananchi tunatamani kuendelea kujenga taifa letu kwa uhuru na amani, kama ilivyo desturi ya Tanzania.
Ni imani yetu kwamba chini ya uongozi wako, Tanzania itaendelea kuwa nchi ya amani, heshima, na usalama kwa wote.

Nakutakia afya njema na uongozi wenye mafanikio.

Soma Pia: Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) yakemea vitendo vya utekaji, ukatiili na mauaji yanayoendelea nchini

Tanzania mb
ele, daima!
 
Na waliotajwa kuhusuka wabanwe pia!
 
Back
Top Bottom