lutajangurwa
Senior Member
- Sep 21, 2019
- 126
- 172
Majuzi nilienda kununua mbolea kwenye Kampuni ya mbolea ETG. Nikaambiwa, mbolea zote zimeandikwa RUZUKU. Hakuna nafasi ya kupata mbolea kwa njia nyingine yoyote.
Ikumbukwe kwamba, wapo wakulima wengi wanaolima mijini. Hawa viwango vya mbolea wanavyotumia ni kiasi kidogo tu. Lakini wamesahaulika. Mbaya zaidi, hakuna tena uwezekano wa kupata mbolea kama wewe siyo wa kijijini. TUNAOMBA Waziri alione hili.
Namuomba mheshimiwa Waziri, kama hakuna uwezekano wa wakulima wa mijini kupata mbolea ya ruzuku, basi lifunguliwe dirisha dogo kwa ajili ya bei za kawaida. Hili dirisha kwa sasa limefungwa kabisa. Tutaponea wapi?
Ni muhimu kwa Waziri kujua kwamba, hizi mbogamboga na matunda kwenye masoko mengi ya mjini, vinalimwa mjini au pembezoni mwa miji. Kuna wajasiriamali wa maua, nao pia ni wengi wanaotumia mbolea. Tunaomba tusaidiwe ili huduma hii iendelee.