Ombi langu bei za mazao na vyukula vipande maradufu

feisar wa moro

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2020
Posts
365
Reaction score
858
Wakuu hili ni wazo langu kutokana na gharama za uzalishaji kuwa juu itafaa bei za vyakula na mazao mengine zipande ili kumsaidia mkulima..

Haya ni baadhi ya mabadiliko ya gharama za kilimo msimu huu ukilinganisha na msimu uliopita kwa hapa nilipo na hapa nazungumzia zao la mpunga

-Kukodi shamba ni laki 2 kutoka laki 1 msimu uliopita
-Kuandaashamba kwa ajili ya kupanda ni laki moja na 40 kutoka 80elf
-Kupanda ni laki moja na 20 kutoka 80elf
-Mfuko wa mbolea ya kukuzia 50kg ni laki moja na 70 kutoka 80elf
-Ya kuzalishia ni laki na 20 kutoka 60elf
-Gharama za palizi zimepanda mara mbili ya msimu uliopita
-Gharama za uvunaji,usafirishaji mazao imeongezeka mara tatu ya msimu uliopita

Kifupi ni kwamba gharama za kilimo zimeongezeka mara mbili ya misimu iliyopita SASA ILI MKULIMA APATE FAIDA NI LAZIMA BEI ZA VYAKULA ZIWE JUU
 
Hiyo sasa Ni mbaya zaidi, ilipaswa uombe serikali kudhibiti mfumuko.

Mfumuko ukiendelea hivyo uchumi unaanguka.unakua na mil 1 mfukoni alafu huwezi kufanyia manunuzi yoyote.
 
Huu mfumuko wa bei ni dunia nzima sidhani kama Tanzania itaweza kuudhibiti ikiwa dunia nzima inapitia hii hali
 
Wakuu hili ni wazo langu kutokana na gharama za uzalishaji kuwa juu itafaa bei za vyakula na mazao mengine zipande ili kumsaidia mkulima..

Haya ni baadhi ya mabadiliko ya gharama za kilimo msimu huu ukilinganisha na msimu uliopita kwa hapa nilipo na hapa nazungumzia zao la mpunga

-Kukodi shamba ni laki 2 kutoka laki 1 msimu uliopita
-Kuandaashamba kwa ajili ya kupanda ni laki moja na 40 kutoka 80elf
-Kupanda ni laki moja na 20 kutoka 80elf
-Mfuko wa mbolea ya kukuzia 50kg ni laki moja na 70 kutoka 80elf
-Ya kuzalishia ni laki na 20 kutoka 60elf
-Gharama za palizi zimepanda mara mbili ya msimu uliopita
-Gharama za uvunaji,usafirishaji mazao imeongezeka mara tatu ya msimu uliopita

Kifupi ni kwamba gharama za kilimo zimeongezeka mara mbili ya misimu iliyopita SASA ILI MKULIMA APATE FAIDA NI LAZIMA BEI ZA VYAKULA ZIWE JUU
kwanini asibuni namna ya kupunguza gharama za uzalishaji, ili wanunuzi wawe na uwezo wa kulipia hiko unachoa zalisha. Gharama hazitashuka milele ubunifu ndio unatakiwa badala ya kununua mbolea si zipo mbolea za asili, nafuu na haziumizi ardhi. Tumia best practices katika kilimo upunguze gharama za uzalishaji badala ya kututwisha sie gharama wenzie tutaomba kibari cha kuagiza kule wanapotumia gharama nafuu.

Wapi unaandaa shamba laki nunua trecta weka lita 5 tu unamaliza eka na chenji inarudi, kuvuna tafuta harvestor kama wewe huwezi ndio mzungumze wakulima wote kijijini mchangie. Ili mkulima apate faida tumia technolojia na best practices.
 
Mkuu asilimia kubwa ya chakula kinacholiwa hapa Tanzania kinazalishwa na wakulima wadogo

Mkulima mdogo ambaye hata bado hawezi kumudu kununua ng'ombe wa kulimia ukimwambia anunue treka au power tille sidhani kama inawezekana kirahisi hivyo

Na kama wakulima wote watatumia mbolea za asili sidhani kama itawezekana hizo samadi kutosheleza mahitaji ya mbolea nchi nzima
 
Basi chukua kutoka field kabisa wengi wa wakulima hao wadogo hawatumii kabisa mbolea na gharama kubwa ni nguvu zao, mbegu wanahifadhi na sio DMO. Sasa mtu mwenye ng'ombe wakichanga wanakosaje tractor, halafu kupanga ni kuchagua sasa tuchague kupunguza gharama.

Wenzio tulichangisha wakulima Kyela wakanunua power la halmashauri kwa kuchangia ile 10%, hawachangii gharama yote ya tractor ni ile 10 - 20% ebu jifungueni katika mawazo mgando na tokeni nje ya box kuweni positive tunakwenda mbele.

Si wakulima wote wanatumia mbolea yapo maeneo ardhi bado haijabadilika ni bikra kabisa wale waliozoea mbolea uweza wa kununua mbolea wanayo ni ruzuku tu na sio kupandisha bei. Point hapa ni kupunguza gharama za uzalishaji, kuongeza tija na kupunguza harvest and post harvest loss. Hii hatukuombi ndio ukweli wakulima wetu wachague ukweli na technolojia.
 
Back
Top Bottom