sembo
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 4,350
- 3,451
Tangu jana kumezagaa tetesi kua, kocha mwenye heshima kubwa nchini Tanzania na katika klabu ya Simba S.C, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ametangaza kujiuzulu ukocha, na kuapa kutofundisha tena mpira nchini Tanzania.
Baadhi ya mambo yaliyompa heshima ndani ya Simba S.C ni;
1. Utumishi wake uliotukuka ndani ya klabu ya Simba S.C.
Julio amewahi kuwa kocha msaidizi, kocha mkuu na meneja wa timu bora kwa sasa katika ukanda huu wa CECAFA, Simba S.C katika vipindi mbali mbali. Na katika mda wote huo, ameipatia Simba S.C mafanikio mbali mbali.
2. Mpira mwingi aliowahi kucheza akiwa na uzi wa Simba S.C.
Julio ameitumikia Simba S.C kama mchezaji, kwa weledi na nidhamu ya hali ya juu. Katika kipindi hiki, Julio alicheza soka la kiwango cha juu sana, hadi kufikia hatua ya kukabidhiwa "kiti" cha kudumu katika historia ya mabeki visiki kuwahi kushuhudiwa nchini.
3. Kauli zake za vitisho na tambo kwa timu pinzani ambazo zilikua zikitupa ushindi kabla hata mechi haijaanza na hasa hasa kwa wale jamaa wa nibebeee.. nibebeee..
Moja ya kauli yake ni hii.. "Nakuambia hao Yanga hawana tofauti na mwembe wa uani, unatingisha unakinga kapu lako unachukua matunda."
Ombi langu kwa Jamhuri Kihwelo 'Julio' ;
Kama ulivyoona ya 01.10.2016 japo.. jamaa walibebwa hadi kinyaa.. hatukukimbia uwanja, tulipambana hadi dakika ya mwisho.
Kukaa pembeni si njia ya kusolve tatizo.. rudi uwanjani tupambane.
Julio, soka la Tanzania bado linakuhitaji sana.. Simba S.C bado tunakuhitaji sana.. kunjua moyo kaka.
SIMBA S.C, NGUVU MOJA.