Ombi langu Maalum kwa Mhe Rais:Naomba uwaachie Rais wa DARUSO na Katibu wa TGNP

Mkuu Gembe, umeeleza vizuri. hawa vijana na hata mabango yao wala si ya uchochezi bali ni kufikisha tu ujumbe walionao kwa jamii ni kama tu magazeti. watanzania tuna uhuru wa ku eleza matatizo yetu pasipo kubughudhiwa na mtu yoyote. hapa ni hasira tu za uongozi wa chuo ndiyo zinasababisha wanafunzi wateseke, hii ni mbaya sana.
hata hiyo kesi itafutika tu mbona zile za mwaka jana zilifutika baada ya kuona makosa ya wanafunzi yanatakiwa yasikilizwe na uongozi wa chuo na wapewe adhabu na chuo?
 
Unaweza kutusaidia kifungu cha Katiba (ya Marekani) alichotumia Rais Obama? ... siamini kama alikurupuka tu ... na hiyo Guantanamo Bay iliundwaje na kwa mamlaka ya nani?

Mkuu Ilongo,

Obama ameingilia suala la Guantanamo Bay,nakuamuru kesi hizo za Kijeshi zisimamishwe kwa kuwa Obama kama Rais wa Marekani kikatiba ndiye amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya Marekani.Kiprotokali Obama ameamuru kesi za kijeshi za Guantanamo Bay zisimamishwe ili mchakato wa kesi hizo upitiwe upya.So anayo mamlaka kwa sababu suala lenyewe ni la kijeshi,but in our case ,Udsm Student's Saga is totally different.Norma legal procedure should be adhered.Hapo ndipo kuliko na tofauti kati ya hizi ishu mbili

Ndiyo maana naona kama Jk tunampa fursa ya kuingilia mahakama zetu,au kuendesha mahakama za kiraia as if ni za kijeshi.Ndiyo maana kule Mara nilipinga Suala la Lowasa pia kuamuru polisi kuachia raia waliokua wamekamatwa wakiwa na mabango.Nilipinga nikasema huo uwezo Lowasa aliutoa wapi kisheria.Hata kama alikua waziri mkuu.Yes alifanya jambo jema kuwanusuru wale waliokua wananyanyaswa,lakini je kama tulimsifia alipoamuru mtu kuachiwa huru,je asingeutumia huo uwezo wakati mwingine kuamuru mtu kukamatwa?

Au kwa hii kesi kama anaweza kuamuru wanafunzi wa UDSM waachiwe,je huoni anaweza kutumia uwezohuo kuamuru watu wakamatwe,au nwaliowekwa detention kama ni mafisadi au maswahiba wake waachiwe?
 


Mkuu Gembe,

I beg to differ with you, Je, unataka kuniambia kuwa katiba ya nchi hii inampa mamlaka Rais kuwasamehe watu ambao wanatuhumiwa kufanya makosa? Kama hana uwezo wa kufanya hivyo kikatiba kwanini unamwomba? Let hao vijana wa-face hizo charges na kama inatakiwa msaada basi ni pale Kisutu. Tuweke standards za kurejesha nidhamu na utawala bora. Kufikishwa Kisutu ndiyo mahala muafaka zaidi badala ya kuomba kuvunja sheria.
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…