Mi mi
JF-Expert Member
- Jul 14, 2024
- 2,748
- 5,112
Mmmh, Haleluya
Huwaapia moyo
Nitakulinda
Maana najua kwamba kuna chemichemi
Nitakujengea boma uwe salama
Adui akija asikuweze
Usiruhusu maneno yakuvuruge
Usiruhusu hasira ikae kwako
Namuweka mlinzi awe ngome yako
Akupiganie ubaki salama
Bwana naomba utete nao wale
Wanaoteta nami
Naomba upigane na adui zangu wote
Mimi sitaki kubishana nao
Sitaki kupambana nao
Nisije nikakosea wakanilaumu
Maana wameshavuta upinde
Wapo kwenye mangojeo yao
Wamenuna wamekunja sura wana hasira nami
Kinachowafanya wasinidhuru ni kwamba hawajapata sababu
Wanahesabu hatua zangu nikosee waninase
Usiache mguu usogezwe unase kwenye mitego yao
Weka mngozeji kinywani mwangu anilinde nisiropoke
Heeeeeee
Hili ni ombi langu kwako
Mungu akukumbuke na wewe
Katembee na wewe ( Katembee na wewe )
Katembee na wewe ( Atakuwa mboni zangu akulinde )
Moyo wangu ( Wewe ni wimbo wangu )
Wewe ni bwana wangu ( Tena dawa ya moyoni mwangu )
Wewe u fahari yangu ( Ufahari yangu )
Wewe u ukuta wangu
Wewe u thamani yangu (Atakuwa mboni zangu akulinde)
Wewe u mwaminifu wangu
Bwana wewe unaweza (Aaaaaaaa)
Wewe ni Mungu uliye hai (Aaaaaaaa)
Wewe ni mfalme wa ajabu
Wewe unayeponya mioyo
Halleluya
Nifanye kama Yusufu
Uliyemwona mwota ndoto ukambariki
Wewe ulimwona waziri mkuu
Tofauti na wanadamu
Wakamtazama vingine walivyoweza
Baba yake alimwona mpelelezi awapeleleze ndugu zake
Ndugu zake walimwona ni mbeya wakamtupa shimoni
Wamidiani wakamwona biashara wakamuuza kwa Potifa
Mkewe Potifa kamtamani akamwona kijana mzuri
Wafungwa wenzake wakamsahau wakifikiri ni mwarifu
Wewe uliona ndoto ndani yake ukamfanya waziri mkuu
Na mimi nifanye kama Yusufu
Hili ni ombi langu kwako
Mungu akukumbuke na wewe
Katembee na wewe ( Katembee na wewe )
Katembee na wewe ( Atakuwa mboni zangu akulinde )
Moyo wangu ( Wewe ni wimbo wangu )
Wewe ni bwana wangu ( Tena dawa ya moyoni mwangu )
Wewe u fahari yangu ( Ufahari yangu)
Wewe u ukuta wangu
Wewe u thamani yangu (Atakuwa mboni zangu akulinde)
Wewe u mwaminifu wangu
Bwana wewe unaweza (Aaaaaaaa)
Wewe ni Mungu uliye hai (Aaaaaaaa)
Wewe ni mfalme wa ajabu
Wewe unayeponya mioyo
Wewe ni kisima kwako nitachota hekima
Kwako nitachota baraka
Kwako nitachota wema
Kwako nitachota ukuu
Kwakoo ooh, kwako nitajifunza
Kwako nitaburudika
Aaaaaah Aaaaah Aaaah Aaaah
Jina lako messiah
Hili ni ombi langu
Nifundishe kuomba
Nifundishe kunena
Nifundishe kiasi
Nifundishe imani ya
Matendo, nipe moyo wa toba
Nautaka uwepo wako unakoishi
Ambako wewe ni kichwa cha kanisa
Nazitaka nguvu, ulizonazo wewe ninataka upako
Maneno yangu, matendo yangu, tabia yangu
Zifanane na hisia zako
Nikitembea nitembee na wewe Yesu
Ninataka kushinda aaaiii
Nami nakusalute eeh master
Ninakuimbia wimbo, ninapaza sauti
Nami na kusifu, kuhani wa ubora
Mmiliki halali kwa agano la neema
Jina lako ni messiah
Hili ni ombi langu, nifundishe kuomba
Nifundishe kunena, nifundishe kiasi
Nifundishe imani ya matendo, nipe
Moyo wa toba
Ndani ya moyo wangu, ninataka uishi wewe bwana wa wema
Uewezae kuuzuia ulimi wangu
Usinene sawasawa na hasira zangu
Uewezae kuituliza akili yangu
Isichanganyikiwe wakati wa raha
Uwezae kunituliza wakati wa shida na matatizo
Wakati wengine wakimbiapo, ukanipe
Jibu la mbio zao
Nguvu yako ikanizuie kwenda pale hakuna
Awezae nion pale ambapo
Hayupo awezae
Sema acha, neon lako likanizuie kufanya
Neema yako Ikanifanye kupakua
Chakula tofautu Na njaa yangu
Kule nisikoweza Kwenda mchana
Nisaidie nisiende usiku
Yale nisiyoweza, Sema hadharani, Nisiseme gizani
Nautaka uso wako Kama wa chuma
Vinyamkela wasioweza Kuustahimili
Naitaka lugha ya Kimbingu, isiyoneneka
Isiyonenwa na mtu
Natamani mbingu Za mbingu kwenye
Neema, kule Paulo Alipoogelea nguvu zako
Nikitembea, nitembee Na wewe Yesu
Ninataka kushinda aaaaiiii
Nitakanyaga mahali waoga hawapawezi
Nitafanya ubabe Kwenye ulimwengu Wa roho
Nitapitisha mkong'oto Kwenye mikwamo
Nitaonyesha jeuri Kwa shetani
Maana ufalme Nauteka oooo
Unatekwa na wenye Nguvu aiiiii
Nami nakusalute Ninakuimbia wimbo,
Ninapaza sauti Nami nakusifu
Kuhani wa ubora
Mmiliki halali wa
Agano la neema
Jina lako ni Messiah
Hili ni ni ombi langu
Nifundishe kuomba
Nifundishe kunena
Nifundishe kiasi
Nifundishe imani
Ya matendo, nipe Moyo wa toba