Ombi langu TFF, Waamuzi wa Kike wasitumike kwenye ligi yetu

Ombi langu TFF, Waamuzi wa Kike wasitumike kwenye ligi yetu

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
10,677
Reaction score
11,768
Japo nitaoneka sijui kitu, ama nataka kuharibu vibarua vya watu, lakini angalau na mimi nitoe dukuduku langu.

Kwakweli TFF angalieni namna nyingine ya kuwatumia waamuzi wa kike, ama watumike kwenye mechi za wanawanake wenzao ama wawe washika vibendera wa pembeni (tena hapa upite mchujo) ila kuchezesha kama marefa wakati kwenye mechi za wanaume tena kwenye mechi yenye pressure kama ya jana mnakosea.

Sipo kumdharau mwanamke, hapana, lakini marefa wetu wakike wameonesha hawawezi kuhimili pressure ya michezo, sio jana tu, nimeona kwenye mechi nyingi tu.

Jana Refa alionyesha game kumshinda, kwangu nimemuhukumu kwa uwanawake wake sio chochote.

Japo huko Ulaya wanawake huwa wanachezesha mechi za wanaume, lakini sio kwenye game zenye pressure. Tena hata hizo mechi za kawaida sio kila mara kama huku kwetu.

NbB: Mchimbaji nae anamawazo, asidharauliwe.
 
Walifanya makusudi kumuweka yule wakijua atawabeba makolo, angalia hapa kavaa kabisa jezi ya mbumbumbu fc
F3OibCbWIAAk3AD.jpg
 
Utawalisha wewe..wakikuambia tu tuma na yakutolea unalalamika
 
Nchi hi Ina mambo ya ajabu San ligi za France ,Spain ,england hakuna marefa wa kike Hakuna

Ila huku siasa wako ,mmkp mtu anakuwa makamu rais Kisha rais ,mwingine mwalimu Hadi spika
 
Naunga mkono hoja. Maana kuna mambo wanaweza fanyiwa ikawa kama udhalilishaji tu dhidi yao.

Kumbe angefanyiwa mwanaume ingekua poa tu.
 
Mtu awe mwamuzi kwa ubora na uwezo wake sio jinsia
Me naamini kuna wanawake ni waamuzi wazuri kuliko wanaume
Lakini sio kuwabeba wanawake kisa ku balance jinsia
Wanaume waamuzi bora waamue michezo
Vilevile wanawake wamuzi wazuri waamue michezo
 
Mimi sioni mantiki ya wanawake kuchezesha ligi kuu ya wanaume, na wakati kuna ligi yao ya wanawake. Kama ni hivyo basi na wanaume wakachezeshe kwenye ligi ya wanawake.
 
Hawa marefa wa kike ni Supu za Viongozi pale TFF hawawezi shindwa kuwapa kazi kazma hizo...
Kwahyo tuendelee kuugulia maumivu tu
 
Binafsi sijawahi kumwamini mwanamke kwenye mambo serious. Mke wangu mwenyewe huwa namshirikisha mambo machache mno, tena yanayoendana na akili yake. Nawashangaa wanaume wnzangu wanaokubaliana na upuuzi wa kumshiikisha mke kila kitu.

By the way,New World Order imeharibu mambo mengi sana, inalazimisha mwanamke afanye kila kitu anachokifanya mwanaume. Sipendi kuwaona wanawake kwenye soka.
 
Wakachezeshe netball huko mbona sie kwenye shuhul zao kama kitchen party hatuendi
 
Derby ni mlima mrefu kwa refa wa kike hilo liko wazi!
 
Back
Top Bottom