Ombi Maalum kwa Rais Magufuli: Mteue Zitto Kabwe kuwa Mbunge wa Bunge la JMT, ndiye mpinzani pekee mzalendo, Capable kuongoza PAC!

Huyo si ndio mwenye msemo " nchi imekabidhiwa kwa washamba"
Acha akae mtaani atuonyeshe huo ujanja wake.
 
Samahani mkuu, wakati unaandika hii mambo ulishatumia kinywaji gani?
 

Juhudi za ZZK za kulihujumu taifa letu sio za kufumbia macho hata kidogo! Yeye na nyoka wengine wa aina yake hawastahili hata ujumbe wa nyumba kumi!
 
CCM inavituko Kwahiyo hawakujua kama hizo kamati zina takiwa kuongozwa na upinzani Leo hii zito ateuliwe kama mpinzani bungeni hahaha inachekesha sana si mlitaka muwe pekee bungeni Sasa pilipili inawawashia nini?
 
Mnawaumiza sana akina Mbowe na Lissu nyie jamaa Pascal pata tot 2 hapo dukani ndugu yangu
 
Bandiko MOTO....😍😍

Binafsi ninaunga MKONO HOJA.....

Mh.Zitto Kabwe amejipambanua kuwa MWANASIASA flexible sitaki kusema kuwa ni mzalendo zaidi,laa hasha maana ninaamini WANASIASA wote walio vyamani ni WAZALENDO kwa sababu ya kusajiliwa kihalali.....

Kongole kwa Mh.Zitto Kabwe kwa kumuelewa vyema hayati BOUTROUS BOUTROUS GHALI(UN SG) na Yale maneno yake kuntu kuwa "only stupid people, do not change their minds".

Kongole sana kwa mh. ZZK na ACT kuifikia SUK....

Nakuunga mkono PM kwa pendekezo muruwa la mh. Zitto kuwepo ndani ya BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ili aendeleze KUCHANGAMSHA fikra TUNDUIZI.



Kijana muuza Al Kasus
Tandale
 
Zitto hata akiteuliwa kuwa mtendaji wa kata atakubali haraka sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…