Ombi Maalum kwa Rais Magufuli: Mteue Zitto Kabwe kuwa Mbunge wa Bunge la JMT, ndiye mpinzani pekee mzalendo, Capable kuongoza PAC!

Kwanza kabisa, ubunge wa kupewa na rais ni ubunge wa kwenda mtumikia rais na sio wananchi au waandishi.
Pasco Mayalla sio mtu sahihi kabisa kuwawakilisha waandishi, ni mchumia tumbo na mlamba viatu vya watawala wa kiCCM.

Mtu aliyesababisha Eric Kabendera kuwekwa kizuizini mpaka akapoteza mama yake mzazi, leo hii mtu huyo awatetee waandishi? Thubutu.
 
Mkuu Paschal Mayalla,

Kwa mara ya kwanza nakupinga kwa hoja hii, that is a nasty fox to bring in the folk. Whatever reasons you might paint on Zitto it will discredit yourself, plerase distance yourself from a man who acts like a serpent flaming fire of abyss.

I value your constructive opinions and intellectual reasoning, but on this I can't be part of the contributory negligence towards the doomsday.

Big NO
 
THREAD IMEKAA KINAFIKI KIKUDA!

MAYALA NI "njaa" 🤣🤣🤣🤣
 
Amteue nani? Mbona nchi itanuka? ZZK hakubaliki kwa yeyote anayemfahamu. Msiomfahamu ndio mnadhani anafaa kuaminiwa. Hafai.
Nakubali alipokuwa mwenyekiti PAC alikuwa akiomba rushwa sio mchezo niu mla rushwa wa kutupwa

Asingekuwa mpenda rushwa angekuwa mbali kisiasa lakini looo asione hela.Yeye na Lisu ni wapiga mikelele tu lakini ni wala rushwa hatari
 
Unawezaje kuweka gunzi katikati ya betri mbili? Tochi itawaka?

Watanzania siyo wajinga, mmeachiwa bungenna serikali muendeshe wenyewe wala msitafute watu wa kuwasingizia kwamba waliwakwamisha

Mtaani huku bei ya mafuta ya kula dumu la lita 20 ni sh 80,000/= bei ya leo hiyo, cement ndio sitaki hata kuuliza bei.

Mlitaka bunge la kijani hilo mmeachiwa msitafite mtu wa kumsingizia failure zenu.
 
Pascal Njaa una kazi kweli ? Utaalam wa mambo ya njaa unao ? Utaalam wa kupiga ramli chama gani kinaenda kuwa chama kikuu cha upinzani unao ? Utaalam wa kumshauri Jiwe nao unao ? Kujidai unajua kila kitu ? Wakati hamna lolote .
 
BROTHER, kwanza hongera kwa uchambuzi makini, lakini nina maswali kwako kwa kuwa mimi binafsi nishindwa kupata majibu:-
  1. Hivi inawezekana mkubwa akiwa hajakomaa watoto wawe wamekomaa?
  2. Unaamini matendo ya chama tawala ni matendo ya chama kilichokomaa?
  3. Baada ya uchaguzi huu bado unaamini kuna chama cha siasa kilichoko komaa hapa TZ Hasa ukihusisha matendo yaliyoambatana na mwenendo mzima wa uchaguzi uliopita
  4. Kwa kupima kwako kati ya uchaguzi huu na ule wa mwaka 2010 na 2015 unaona tumeenda mbele ama tumerudi nyuma katika kukomaa kwa demokrasia yetu?
  5. Unaweza ukatufahamisha kwa sasa tunaelekea wapi juu au tunapolomoka?
  6. Kwa sasa unaliona taifa hili liko katika hali ya kawaida? na kama sio kwa nini?
  7. Ni nini kimetufikisha huku ? ni hao wasio komaa au ni huyo aliyekomaa?
  8. Matendo ya aliyekomaa yako sawasawa na ukomavu wake?
  9. Kukomaa maana yake ni kukubaliana na matendo yasiyokuwa ya kikomavu ili uonekane umekomaa?
  10. Unaielewa hukumu iliyo ndani ya mioyo ya watanzania kuhusu huyo unaedhani amekomaa,ameyaponya vipi majeraha ya walioumia,kutwezwa,kulia,kuomboleza nk ambao sasa wanamuona amewaacha ili akale kuku kwa mrija,anayo maneno ya kuwa laghai hao watu na waelewe kuwa kaenda pale kuteseka kwa ajili yao na si kustarehe?
Kaka ukomavu wa wanasiasa wa vyama vichanga utausoma kutoka kwenye matendo ya chama kilicho komaa. Kuna ukomavu unaozidi kuvumilia zuio la kufanya siasa kwa muda wa miaka mitano kinyume cha sheria za nchi na katiba,harafu unatuambia huyu anaezuia wenzake amekomaa kuliko walio zuiwa, hii sio haki brother,najua unajua isipokuwa basi.
Ni mimi Ngedelewaulaya naludi zangu poli majibu yangu ntayafuata kesho.
 
Kuhusu hawa wenyeviti wa PAC ni wala rushwa hatari. Kuanzia dr slaa, zito na wenzake wote mavi tuu wanafiki balaa watumishi wa halmashauri wanawajua vizuri hawa mafisidi.
 
Kwani walishindwa nini kumuachia Seif awe Rais Zanzibar wakati jeshi bado liko chini ya Rais Wa JMT!? Seif anaweza kuvunja muungano na huku hana jeshi!? Kilichofanyika ni kuunga mkono kupindua maamuzi ya wananchi wa Zanzibar na hiyo ndiyo imetoka. Katu ccm haitakaa tena iogope kufanya faulo za uchaguzi kwa kuwa wanajua vyeo vitawarudisha tu serikalini.
 
Zitto akaongoze PAC. PAC hii hii inayokatazwa isiyakague baadhi ya mashirika!? Kwa faida ya nani!?
 
Si vibaya unge declare kwamba jamaa ni miongoni mwa maswahiba zako wa siku nyingi
 

Mkuu, unajua upo uwezekano wa kumponda mtu bila kutumia kinywa chako wewe mwenyewe?

Hapa Mayalla kamponda ZZK bila kutumia kinywa chake mwenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…