Uchaguzi 2020 Ombi mahsusi kwa uongozi wa CHADEMA Media juu ya hotuba za Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Ombi mahsusi kwa uongozi wa CHADEMA Media juu ya hotuba za Tundu Lissu

kindafu

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Posts
1,346
Reaction score
1,678
Please uongozi wa CHADEMA Media fanyeni hima hotuba zote za Lissu kila anakofanya mkutano zitengenewe clips za peke yake kuwezesha wadau mbali mbali kuweza kufuatilia kwa mtiririko hotuba hizo.

Pia itarahisisha kuzisambaza kwa umma kupitia ma group ya WhatsApp na mitandao mingine! Vipande mnavyorusha YouTube vimekatwa katwa na mara nyingi mtu hupati hotuba nzima.

Binafsi nimetamani kuisikia hotuba kamili ya Lissu Arusha lakini napata vipande tu! Amkeni tafadhali - mmezuiliwa kuonekana kwenye Runinga, msizubae kutufikia kwa njia nyingine mbadala kupitia CHADEMA Media!
 
Pesa za Michango hamjatoa na hamtoi halafu tena mnataka muwekewe kila Kitu Mitandaoni. CHADEMA sasa wana 'Umasikini' ulio wa ghafla sana.
 
Hahahhaa Kama hata Hili Hawawezi Wataweza Ongoza nchi kweli hahahh
 
CHADEMA hawajajipanga kwenye huu uchaguzi, kama upo makini utaona kuwa kwa upande wa upinzani ACT wapo makini zaidi.
 
Pesa za Michango hamjatoa na hamtoi halafu tena mnataka muwekewe kila Kitu Mitandaoni. CHADEMA sasa wana 'Umasikini' ulio wa ghafla sana.

Hapa kweli wandugu. Tulio na mapenzi mema kwa hiki chama, na tunaotaka mabadiliko, tujichange jamani.

Nahisi hawawezi tu kuweka wazi kila kitu, ila itakuwa wamebanwa mno kifedha ili wasipate pakupumulia kabisa.
 
Hapa kweli wandugu. Tulio na mapenzi mema kwa hiki chama, na tunaotaka mabadiliko, tujichange jamani. Nahisi hawawezi tu kuweka wazi kila kitu, ila itakuwa wamebanwa mno kifedha ili wasipate pakupumulia kabisa.
Hivi hata kutoa taarifa kwa umma tabu. Hawana hata kamera za kurekodia. Duh, Lissu angejua angejiunga ACT. Hiki chama kimejaa wazee wa visusio ni balaa
 
ACT ndio Kifo Cha CHADEMA NA WALA SIO CCM wait and See.
 
Back
Top Bottom