OMBI: Serikali ingilia kati biashara 'mpya' ya Forex

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Kwanza nianze kusema kwamba sina neno baya na mtu yeyote anayejihusisha au kufundisha biashara hii. Ni biashara inayoweza kuwa mkombozi mkubwa kama itafanywa kwa ubunifu, umakini na uangalizi mzuri. Nitaelezea wasiwasi wangu na mawazo yangu ya nini kifanyike HARAKA.

Tumeona biashara nyingi tu mpya ambazo kwa nia nzuri tu, serikali iliziacha zikue bila kuziingilia halafu sheria na miongozo mbalimbali ikatungwa baadae kulingana na changamoto na hali halisi ya hiyo biashara ilivyokuwa. Biashara kama ya bodaboda ni mfano halisi. Na hata drone operation ni biashara nyingine ambayo kwa nia nzuri tu, imeachwa ingawa najua huko mbele mambo yatabadilika. Tofauti na biashara zingine ambazo mara nyingi serikali imekuwa inaziacha zinaanza, na kuzipa muda wa kuji-establish, Forex ina tatizo moja kubwa. Yoyote anayeshiriki anaweka hisia zake kubwa sana kwa hiyo mtu anaposhindwa maumivu yanakuwa makubwa kisaikolojia na hata kimwili. Tusiache kama tulivyoacha biashara ya bodaboda, mpaka watu wapate vilema vya maisha na vifo vinavyoweza kuepukika kwa kuweka tu miongozo na kuisimamia.

Kuna baadhi ya watu bila kutajana majina wamekuwa vinara wa kupromote hii biashara. Binafsi nawapongeza siyo tu kwa jitihada za kusaidia wengine kuinuka kiuchumi lakini hata na wao wenyewe kwa kuona fursa na kuitumia. Nina uhakika kuna watu tayari wamefaidika na mafanikio yao.

WASIWASI WANGU

Tatizo zangu kubwa linakuja kwenye issue nzima ya usajili na regulation ya forex brokers. Sina uhakika brokers wanaofanya online Forex trading wamefika wangapi mpasa sasa hapa Tanzania, ila utapeli wa kwanza kwenye Forex kawaida unaanzia kwenye brokers.

Ni standard practice kwa trainer au training material yoyote inayohusiana na forex trading kuonya kuwa biashara ya Forex trading ina risk kubwa na unaweza kupoteza hela yako yote. Wenyewe wana msemo mmoja, 'only invest money that you can afford to lose'. Ni msemo ambao ningependa tupate tafsiri ya kiswahili kwa sababu unakuambia kila unachohitaji kujua kuhusu risk iliyopo kwenye biashara hii. Kuna na msemo mwingine wanautumia unasema 'past performance is no guarantee of future results'. Huu wanauambatanisha kwenye kila 'evidence' au ushuhuda wa matokeo mazuri kwenye trading. Nadhani hii misemo ni sehemu ya kutimiza masharti ya sheria zinazowaongoza?. Kwa kuwa sisi Tanzania hatuna muongozo wowote mpaka sasa, hata hii misemo hamna anayeona umuhimu au mwenye ufahamu wa kuhakikisha anaiambatanisha kwenye hizo screenshots au kabla ya kutoa mafunzo au marketing yoyote inayohusiana na forex trading.

Kuna broker mmoja ambaye tayari anafanya shughuli zake Tanzania nimejisajili kwake na nimeshafanya trade kadhaa, naendelea kukusanya ushahidi wa utapeli anaoufanya na nitauleta hapa wiki ijayo.

MAPENDEKEZO

Wazungu wanasema, 'the genie is already out of the bottle'. Badala ya kuanza kufikiria kuipiga marufuku hii biashara ambayo kama nilivyotangulia kusema, ikifanywa kwa umakini, inaweza kuwa na mchango mkubwa kwa taifa hili, ni vyema tukaangalia nini kinaweza kufanywa kuepuka utapeli na pia kuhakikisha inawafikia ipasavyo wale wanaoweza kufaidika nayo.

Pendekezo la kwanza. Chombo cha mpito kianzishwe mara moja kitakachoratibu shughuli nzima ya Forex trading Tanzania. Maeneo muhimu yanayohitaji uangalizi wa haraka:
  • kuratibu mafunzo yote ya Forex trading yanayotolewa na watu, taasisi na makampuni mbalimbali. Hii ijumuishe utoaji wa gharama elekezi, muda stahiki wa mafunzo na hata certification kwa wale wanaofuzu.
  • kuratibu uendeshaji wa brokers wote waliosajiliwa Tanzania. Hii ijumuishe kufuatilia utendaji wa kazi wa brokers kuhakikisha hawafanyi utapeli wowote wakati wa kuexecute orders na pia malipo kati ya brokers na traders yanafanyika bila matatizo.
  • jukumu la kupokea malalamiko yoyote ya kutoka kwa traders kuhusu broker yoyote na kuyafanyia kazi (sasa hivi ukitapeliwa na broker hivi unaanzia kwenda wapi?).
Pendekezo la pili. Taasisi mbalimbali za elimu kama IFM, CBE na hata Open University waanzishe short Certificate programs, kama ya 'Investment and Portfolio Management', ambapo humo humo kutakuwa na mafunzo ya Forex Trading.

Pendekezo la tatu. Tusukume tuwe na home-grown Forex brokers. Tayari kuna stock brokers, ni suala la kuwapa incentives mbalimbali hao hao ili watoe huduma ya online forex trading (ambayo by extension pia mtu utaweza kutrade online hata hisa zilizopo kwenye Dar es Salaam Stock Exchange). Sasa hivi kijana wa kitanzania aliye Tandale ni rahisi kununua hisa za facebook na McDonalds kuliko za CRDB au TBL. Hili ni la kuangalia haraka.

Pendekezo la nne. Wadau mbalimbali wapewe motisha ya kuandika na kutafsiri makala na vitabu vya kuhusu Forex trading kwa lugha ya Kiswahili. Mimi nina uhakika itafika wakati hata muendesha bodaboda anaweza kuifanya hii biashara akipewa mafunzo katika lugha na mazingira rafiki.


Post yangu pekee niliyowahi kuchangia humu kuhusu Forex Trading:
Madini yangu kuhusu FOREX Trading!
 
HONGERA SANA
 
OnTaRio ni Tapeli sana sana, Wengi tuliyajua haya, Kitendo cha yeye kuingia mkataba na broker ili kuwaumiza vijana hakikubaliki

Kitendo cha kushindwa kujibu hoja na kutumia matusi anapoulizwa kuhusu huyo tapeli mwenzake broker wa JP ni shidaa
 
Forex, Ni ya ukweli Ila tatizo mtu aliewahamasisha wenzake na hii biashara hana utu yeye anaangalia masirahi yake binafsi zaidi uunguze account usiunguze hana cha kukushauri zaidi ya majibu mabovu yani kwa ufupi we ukiungaza account ye kwake furaha zaidi, inshort yani wewe ndio unakuwa fursa
 
"Men have been trained and conditioned by women, not unlike the way Pavlov conditioned his dogs, into becoming their slaves. As compensation for their labours men are given periodic use of a woman's vagina." The book contends that young boys are encouraged to associate their masculinity with their ability to be sexually intimate with a woman, and that a woman can control a man by socially empowering herself to be the gate-keeper to his sense of masculinity. Vilar states that this has been going on for some time.
 
Forex si kitu kipya hebu ficheni ujinga .. sema ni kitu kigeni kwenu
Nimegundua wabongo bado sana,yaani FX toka waijue utadhani ni kitu kipya,halafu eti humu kuna wasafiri,wasomi ila hii kitu FX imewatoa kapa,dah ila si mbaya imejulikana,na mbongo akijua kitu mtamkoma
 
Source
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…